Wananchi wa Kijiji cha Mkungugu jimbo la Ismani katika
Halmashauri ya Wilaya ya Iringa mkoani Iringa wakiwa katika foleni ya kupiga
kura ya kumchagua Mbunge wao katuika uchaguzi mdogo uliyofanyika leo Juni 01,
2026.
Mwananchi Mkazi wa wa Kijiji cha Kihongorota katika Halmashauri ya
Wilaya ya Iringa mkoani Iringa, Angelista Mwenda akipiga kura katika uchaguzi
mdogo wa Ubunge jimbo la Ismani uliofanyika leo Juni 01, 2026.
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi,
Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele akipita kuingia katika kituo cha Kura cha
Ofisi ya Kijiji Mtera katika jimbo la Ismani Wilaya ya Iringa mkoani Iringa
kukagua mwenendo wa zoezi la kupiga kura kwa wananchi wa Ismani lililofanyika
leo Juni 01, 2026.
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi,
Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele akizungumza na Mawakala katika moja ya vituo alivyotembelea.MWENYEKITI wa
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Jaji wa Mahakama ya Rufaa Mhe. Jacobs Mwambegele
amesema zoezi la upigaji Kura wa Ubunge katika jimbo la Isman katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Mkoani
Iringa na Kata 12 za Tanzania Bara limekwenda vizuri.
Mwenyekiti huyo wa Tume Jaji Mwambegele amesema hayo leo Juni 01,2026 akiwa katika ofisi za Kijiji Igingilanyi Wilayani Iringa mara baada ya kutembelea na kukagua zoezi la upigaji Kura linavyoendelea katika vituo vya kupigia Kura vya jimbo la Isimani ambako kunafanyika uchaguzi mdogo wa ubunge.
Amesema mwitikio wa wananchi wa Ismani katika kujitokeza kupiga kura umekua mkubwa na hata katika Kata nyingine 12 ambazo nazo zinachagua Madiwani hii leo wamejitokeza kwa Wingi.
Mwenyekiti huyo wa Tume Jaji Mwambegele ameshudia upigaji kura kwa baadhi yavituo vilivyopo katika vijiji vya Igingilanyi, Mkungugu, Kihongorota na Migori.
Kata 12 zilofanya uchaguzi leo ni Mzimuni iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni; Zongomera, Halmashauri ya Manispaa ya Kahama; Itilo, Halmashauri ya Mji Nzega; Ketare, Halmashauri ya Mji Tarime na Nyumbigwa, Halmashauri ya Mji Kasulu.
Nyingine ni Kata ya Kala iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi; Ziba, Halmashauri ya Wilaya Igunga; Kamsisi, Halmashauri ya Wilaya ya Mlele; Nyamugali, Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe; Namasakata Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru; Bwongera, Halmashauri ya Wilaya ya Chato na Kibiti, Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti.

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele akikagua mwenendo wa zoezi la kupiga kura kwa wananchi wa Jimbo la Ismani lililopo Halmashauri ya Iringa mkoani Iringa hii leo Juni 01,2026.
Wananchi wakiwa katika mistari tayari kuingia vituoni kupiga Kura.

0 Comments