SERIKALI imeshauriwa kuangalia uwezekano wa kufanya maboresha katika eneo la daraja la Mfugale lililopo TAZARA jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuondoa msongamano mkubwa wa magari katika kipindi mradi wa mabasi yaendayo haraka utakapo kamilika.
Katika eneo hilo ambapo kuna makutano ya barabara ya Mandela na Nyerere kumekuwepo na msomgamano mkubwa wa magari hali inayosababisha adha kwa watumiaji wa barabara hizo.
Ushauri huo umetolewa leo Machi 29,2023 Wakati Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) ikiongozwa na Mwenyekiti wake Naghenjwa Kaboyoka ikishirikiana na Ofisi ya Taifa ya ukaguzi wa Hesabu za Serikali kufanya ziara ya kutembelea miradi wa ujenzi wa mabasi yaendayo haraka BRT III Gerezani-Gongo la Mboto.
Kaboyoka kwa niaba ya Kamati hiyo amesema wamewashauri Serikali waangalie wanatatua vipi tatizo hilo ili kuondoa usumbufu utakaojitokeza pindi mradi huo utakapokamilika na kuanza kutumika huku akifafanua kama hakutakuwa na ufumbuzi kwenye makutano hayo hata suala la kuwa na mabasi yaendayo kasi inaweza ikawa haina maana.
"Kwa maana kutakuwa na msongamano wa magari mengi na ukizingatia ndo njia ya magari makubwa (maroli) yanayotoka bandarini yanapita hapo,"amesema na kuongeza eneo lingine ambalo waliangalie ni pamoja na sehemu ya kujenga karakana ya BRT III imekuwa na matatizo mengi.
"Wamekuwa wakipata eneo na kuanza shughuli zao na kuondolewa kwa sababu zisizo za msingi na kufanya kutafuta eneo lingine wakati fedha zimeshatumika katika uandaaji wa karakana eneo hilo.Wameenda Killtex wameanza kutengeneza.....wanaambiwa hapana hapa ni kwa mwekezaji mbinafsi.
"Mwekezaji mmoja azuie kazi ambayo imeshaanza ya kutengeneza karakana alafu ihamishwe kwa vile kuna mwekezaji, lakini miaka yote mwekezaji hajafanya lolote, kwahiyo ukiangalia hapa kuna mchezo mchafu unafanyika."
Ametumia nafasi hiyo kueleza miradi inapoanza lazima ipangwe vizuri ili kuoondokana na changamoto ambazo mwisho inaleta changamoto ya kulipa fedha nyingi pasipo sababu na miradi inashindwa kuendelea bila sababu maalumu.
Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa TANROADS Mhandisi Rogatus Mativila amesema mpaka sasa mkandarasi yupo kwenye asilimia 5 na alikuwa anatakiwa kuwa katika asilimia 15 hivyo mkandarasi huyo ameahidi kuhakikisha anaziba gepu la asilimia hizo kwa kufanya kazi kwa bidii usiku na mchana.
Aidha meipongeza kamati kwa kuwasaidia kuwapamaelekezo mbalimbali mazuri ambayo yanwasaidia katika utekelezaji huku akiahidi maelekezo yaliyotolewa na kamati watayatekeleza ukiwemo utaratibu wa kupunguza msongamano TAZARA kama walivyoelekezwa na kushauriwa na Kamati hiyo.
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) ikiongozwa Mwenyekiyti wa Kamati hiyo Mheshimiwa Naghenjwa Kaboyoka wakitembelea mradi wa ujenzi wa BRT awamu ya tatu unaotoka Gerezani-Gongo la Mboto leo Machi 29,2023 Jijini Dar es Salaam.
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) ikiongozwa Mwenyekiyti wa Kamati hiyo Mheshimiwa Naghenjwa Kaboyoka wakitembelea karakana inayotumiwa na mradi wa ujenzi wa BRT awamu ya tatu unaotoka Gerezani-Gongo la Mboto leo Machi 29,2023 Jijini Dar es Salaam.
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MASSAKA WA MMG)
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) Mheshimiwa Naghenjwa Kaboyoka akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea mradi wa ujenzi wa BRT awamu ya tatu unaotoka Gerezani-Gongo la Mboto leo Machi 29,2023 Jijini Dar es Salaam.
Mtendaji Mkuu wa TANROADS Mhandisi Rogatus Mativila akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kutembelea mradi wa ujenzi wa BRT awamu ya tatu unaotoka Gerezani-Gongo la Mboto leo Machi 29,2023 Jijini Dar es Salaam.
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MASSAKA WA MMG)
0 Comments