Dar es Salaam, Jumatano, 7 Agosti 2024 - Benki ya Absa Tanzania leo imetangaza Muhtasari wa Utendaji wa Kifedha kwa kipindi cha Januari hadi Juni mwaka huu. Faida ya benki hiyo imeongezeka kwa 65% ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana.Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Obedi Laiser, alisema kwamba ongezeko hilo la faida linatokana na mazingira mazuri ya biashara, uchumi unaokua, ongezeko la mahitaji ya mikopo, ongezeko la wawekezaji katika vyombo vya kifedha, viwango vya chini vya mfumuko wa bei, na kupungua kwa mabadiliko ya ukwasi katika soko la fedha la ndani na dola ya Marekani. “Benki ya Absa Tanzania ilimudu changamoto hizi kwa ustadi, ikitumia mikakati yetu kuchangamkia fursa zilizopo na kutoa thamani kubwa na suluhisho kwa wateja na wadau wetu wote,” alisema Bw. Laiser.
Laiser aliongeza, “Matokeo haya yanaonyesha dhamira yetu thabiti ya kutoa suluhisho zilizobinafsishwa kwa changamoto za kipekee za ndani na kuendelea kuleta thamani kwa wadau wetu kupitia azma yetu ya ‘Kuiwezesha Afrika ya Kesho, pamoja…hatua moja baada ya nyingine."
Alibainisha kuwa katika nusu ya kwanza ya mwaka 2024, Absa ilizindua chapa yake mpya, ikionyesha mabadiliko kuelekea mtindo wa biashara unaomlenga mteja zaidi, ambao unajumuishwa katika ahadi mpya ya chapa: ‘Story yako ina Thamani.’ “Tumejizatiti kuhakikisha kwamba huduma na bidhaa zote za Absa zinaendana na mwelekeo huu muhimu kuelekea huduma ya benki yenye utu na huruma zaidi.”
“Tukiingia katika nusu ya pili ya mwaka wa fedha, tunabaki na imani na ari ya kuendeleza thamani kwa wanahisa. Benki ya Absa Tanzania itaendelea kuwa na nafasi muhimu katika maisha ya kiuchumi ya watu binafsi, biashara, na kimataifa. Tumejitolea kuunda, kukuza, na kulinda mali kupitia ushirikiano katika maendeleo ya kiuchumi huku tukichangia ukuaji na uendelevu wa Tanzania,” alisema Bw. Laiser, na kuongeza kuwa Benki ya Absa Tanzania inakabili kila changamoto kwa ustadi, ubunifu, na mtazamo chanya, ikitoa suluhisho zilizobinafsishwa kwa wateja wetu.
Akizungumza kuhusu Muhtasari wa Utendaji wa Kifedha, Afisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Bernard Tesha alisema, “Kwa kipindi cha miezi sita kinachoishia Juni 30, 2024, benki ilirekodi mapato ya jumla ya TZS bilioni 105, ongezeko la 25% kutoka TZS bilioni 83.8 za mwaka jana. Faida kabla ya kodi ilipanda kwa 65%, kutoka TZS bilioni 32.7 mwaka 2023 hadi TZS bilioni 54.0 mwaka 2024.
Aidha, jumla ya mali na amana za wateja ziliongezeka kwa 22% na 21%, mtawalia, kufikia TZS bilioni 1,591 na TZS bilioni 1,177. Ubora wa mikopo kwa wateja uliendelea kuboreka kwa ukuaji wa 21.9%, kutoka TZS bilioni 698 mwaka 2023 hadi TZS bilioni 851, huku uwiano wa mikopo isiyolipika ukipungua kutoka 5.8% hadi 4.4%. Mapato kwa Hisa (ROE) yalikuwa asilimia 38.2, juu kutoka asilimia 31.5 mwaka 2023, na kutuweka miongoni mwa bora zaidi katika sekta.”
Bw. Tesha aliongeza, “Mtazamo wetu endelevu wa kutekeleza mkakati wetu wa kidijitali umezaa matunda, na uwiano wa gharama kwa mapato ukiboreka kutoka asilimia 53.5 mwaka 2023 hadi asilimia 46.0 kwa kipindi kinachoishia Juni 30, 2024. Benki imepanuka kupitia njia za kidijitali na kuongeza uwepo wake kwa kiasi kikubwa tangu kuanzishwa kwa huduma za wakala wa benki katika robo ya mwisho ya mwaka 2023, ikiongeza urahisi kwa wateja kote nchini.
Sambamba na mfumo wetu wa Uongozi wa Kijamii na Mazingira (ESG), tulizindua ‘Akaunti ya Absa She’ kusaidia wanawake katika biashara kote nchini kwa kutoa huduma za benki bure na kupanua huduma zetu kwa wajasiriamali wadogo na wa kati (SME), zote kwenye upande wa ufadhili na suluhisho za usimamizi wa fedha.”
Alimalizia kwa kusema kwamba Benki ya Absa Tanzania inatambua umuhimu wa Story za kila mmoja. “Pamoja, tunaunda sura ya kipekee ya mafanikio,
0 Comments