Na: Amina Hezron,Morogoro
Wadau wa zao la Soya kahawa miwa na nyama pori wametakiwa kushiriki kikamilifu kwenye kutoa mapendekezo na maoni yao kwenye Mradi wa Utafiti wa Biashara,Maendeleo na Mazingira (TRADE Hub) ili matokeo yatakayopatikana yaweze kuinua tija ya mazao hayo nchini.
Hayo yameelezwa na Kaimu Rasi wa Ndaki ya Uchumi Kilimo na stadi za Biashara Dkt. Zena Mpendu aliyemuwakilisha Rasi wa Ndaki hiyo Dkt Damas Philip katika warsha iliyoandaliwa na mradi huo ili kuwasilisha matokeo ya awali ya utafiti wao kwa wadau ili kupata maoni yao juu ya namna bora ya kufanya biashara ya haki na endelevu.
Amewataka wadau hao kuzingatia kuwa tasnia hizo zinagusa kwa namna moja ama nyingine maisha na maendeleo ya wadau mbalimbali pamoja na uchumi na maendeleo ya nchi kwa ujumla hivyo watumie fursa hiyo kwa makini kutoa maoni yao ya namna bora ya kuboresha biashara katika tasnia hizo zote za Nyama pori na Mazao ya kilimo.
“Ni vizuri tunaposikiliza hizi mada zinazotolewa tuangalie inaelezea kweli ile hali halisi kwenye maeneo yetu ili tuweze kuboresha yale ambayo tumeyaona lakini pia tuweze sasa kuangalia mapendekezo yanayotoka tuone hayo mapendekezo yatafanyika yanawezekana ili tukitoka hapa tuwe na mapendekezo ambayo ni bora zaidi”, alisema Dkt. Zena.
Dkt. Zena ameeleza kuwa Serikali imekuwa ikiboresha mara kwa mara Sheria, taratibu na Kanuni kuhakikisha kwamba biashara hizo hazisababishi ongezeko la uharibifu wa mazingira na upotevu wa baionuai hivyo ni muhimu kama wadau wa biashara kuhakikisha wanaingia kwenye mikataba ya kijani kwenye biashaa zao ili kuwe na biashara endelevu kwaajili ya watu na ulimwengu pia.
Akieleza malengo ya warsha hiyo Mratibu wa Utafiti na Machapisho SUA Prof. Japhet Kashaigili amesema kuwa ni kuwasilisha kwa wadau matokeo ya tafiti kadhaa ambazo mradi huo umeyapata ili wapate nafasi ya kuyajua, kuyajadili na kutoa mapendekezo ili kuona ni namna gani yanaweza kuchangia kwenye maendeleo ya jamii na Taifa kwa ujumla.
“Lengo lingine la pili la warsha yetu hii na mradi ni kutengeneza mpango au njia itakayotupeleka nchi mahali fulani kuptia ufanyaji wa biashara yenye haki na endelevu nchini Tanzania lakini pia bidhaa zetu ziweze kuhimili ushindani kwenye masoko ya kimataifa na kukuza uchumi”, alifafanua Prof. Kashaigili.
Aidha amesema dhumuni kubwa linalobeba mradi huo ni kuhakikisha biashara ya mazao na nyama pori inakuwa ni injini ya ukuaji wa uchumi jumuishi,Kuondoa umasikini na kama mbinu ya kutekeeleza maendeleo endelevu kama ilivyosisitizwa kwenye Mpango wa maendeleo endelevu bila kuchangia uharibifu wa mazingira.
Kwa upande wake Mkuu wa mradi huo Prof. Reuben Kadigi amesema warsha hiyo ya wadau ni muhimu sana katika kupata maoni na mapendekezo ambayo yatawasaidia watafiti kuweza kutengeneza andiko la sera ambalo litawasilishwa Serikalini ili kusaidia kufikia malengo yaliyokusudiwa.
“Kila mchango wa mdau unaotolewa andika mahali kila ushairi andika ili mwisho wa siku tupate kitu kizuri kifupi cha kuwasilisha serikalini baada ya kufanya uchambuzi wa kina kulingana na matokeo tuliyoyapata maana mwisho wa siku hatuwezi kupeleka kwa watunga sera kitu kinacholeweka nawaweze kukifanyia kazi kwa ustawi wa biashara nchini”, alieleza Prof. Kadigi.

Kwa upande wake Dkt. Charles Malaki aliyemuwakilisha Kaimu Rasi wa Ndaki hiyo amewashukuru wadau waliojitokeza katika warsha hiyo na amewataka kutoa maoni na mapendekezo ya kuboresha matokeo ya tafiti hizo ili kuisaidia Serikali baadae kupata sera bora zitakazosaidia kuwa na uendelevu katika biashara ambayo inajali Mazingira,Nyama pori pamoja na watu.Mradi wa Utafiti wa Biashara,Maendelo na Mazingira (TRADE Hub)ni mradi wa miaka mitano unaotekelezwa na Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kwa kushirikiana na washirika wengine kutoka katika nchi kumi na tano za Afrika, Asia, Uingereza na Brazil kuanzia Februari 2019 hadi Machi 2024.Kaimu Rasi wa Ndaki ya Uchumi Kilimo na stadi za Biashara Dkt. Zena Mpenda akifungua warsha ya Wadau wa Mradi wa TRADE HUB kujadili matokeo ya utafiti.Mratibu wa Utafiti na Machapisho (SUA) ambaye pia ni mtafiti kwenye mradi huo Prof. Japhet Kashaigili akieleza malengo ya Warsha hiyo na kazi ambazo mradi huo umefanya hadi sasa.Mkuu wa mradi wa TRADE HUB, Prof. Reuben Kadigi akitoa neno la ukaribisho kwa Wadau hao kutoka nchi nzima kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufungua warsha hiyo.Dkt. Charles Malaki akitoa neno la shukrani kwa mgeni rasmi na wadau.Picha ya pamoja ya washiriki wa warsha hiyo kutoka SUA na Mikoa mbalimbali ambao ni wadau wa Mazao ya Soya, Kahawa, Mpunga, Parachichi na wawakilishi wa Halmashauri na Makampuni yaliyo kwenye mnyororo wa thamani ya mazao hayo.
Wadau wa Mradi wa TRADE HUB wakifuatilia mawasilisho ya matokeo ya tafiti mbali mbali zilizofanywa kwenye mzao ya Soya, Kahawa,Parachichi,Miwa na Nyama Pori.
0 Comments