About Me

header ads

WATATU WAKAMATWA WAKISAFIRISHA ZAIDI YA KILO 420 ZA DAWA ZA KULEVYA.

 


WATU  watatu wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kibaha Mkoani Pwani wakikabiliwa na mashtaka ya kusafirisha dawa za kulevya aina ya Methemphetamine zenye uzito wa Kilogramu 424.84 pamoja na Heroin Hydrochloride gramu 158.24

Katika hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo na wakili wa serikali Agness Ndanzi imewataja washtakiwa hao kuwa ni Rajabu Kisambwanda (42) mkazi wa Kerege Matumbi, Bakari Said (39) Mkazi wa Kunduchi Mtongani na Hillary Rhite (35) Mkazi wa Kunduchi Sodike.

Washtakiwa hao wanadaiwa kutenda kosa hilo  kinyume na kifungu cha sheria cha  15 (1) (a) na cha (3) (i) cha Sheria ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Sura ya 95 kama illivyorejewa 2019. 

Wakisomewa mashtaka yao  mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Joyce Mkhoi  inadaiwa kuwa, Aprili 10, 2024 huko Zinga Wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani, washtakiwa walikutwa wakisafirisha dawa hizo za kulevya 

Aidha Wakili Ndanzi alidai kuwa, siku na mahali hapo, mshtakiwa Bakari Said (39) Mkazi wa Kunduchi Mtongani alikutwa akisafirisha dawa za kulevya aina ya Heroin hydrochloride yenye uzito wa gramu 158.24.

Hata hivyo washtakiwa hawakuruhusiwa kujibu kitu mahakamani hapo kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi ambazo kwa kawaida husikilizwa mahakama Kuu ama kwa kupewa kibali kutoka kwa DPP. 

Kwa mujibu wa upande wa Jamuhuri upelelezi katika kesi hiyo hado haujakamilika na kesi imeahirishwa hadi Mei, 7 2024 itakapokuja kwa ajili ya kutajwa.





 

Post a Comment

0 Comments