About Me

header ads

KIONGOZI WA BUDDHA ASIFU UHURU WA KUABUDU TANZANIA

Na: Mwandishi wetu - Dar es Salaam, Juni 7, 2026

Kiongozi Mkuu wa dini ya Buddha nchini, Mchungaji Dkt. Ilukuptiye  Pannasekara, amesifu ushirikiano ambao wanaupata sio tu kutoka katika dini zingine bali pia serikalini kwa ujumla.

Ametoa kauli hiyo wakati wa kusherehekea siku ya kuzaliwa kwa kiongozi wa dhehebu la Buddha duniani na uzinduzi wa sanamu ya dhahabu ya Buddha (Golden Buddha Statue) eneo la Upanga jijini Dar es Salaam Juni 7, 2026, ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Mahusiano Mhe. Deus Sangu, akimwakilisha Waziri Mkuu, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba.

Alisema, amekuwa akipata ushirikiano mkubwa kutoka dini nyingine hapa nchini na hivyo kuwafanya waumuni wa Buddha kujisikia furaha.

“Kutokana na mazingira hayo mazuri, tuna jumla ya miradi mitano  kwenye sekta za elimu, utalii na afya, miradin hii tayari mingine imeanza na mingine iko katika hatua mbalimbali.” Alisema.

“Hatuhitaji usaidizi wa fedha kutoka serikalini, tunahitaji ushirikiano, miradi hii mitano ni ya uhakika, italeta zaidi ya dola za kimarekani milioni 100 kwenye uchumi wa Tanzania, alisema Mchungaji Dkt. Pannasekara.
Kwa upande wake, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Deus Sangu, amewahakikishia kuwa Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wake, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, itaendelea kutoa ushirikiano kwa dini zote bila kuwepo kwa ubaguzi.

Amesema Muelekeo wa serikali inapoanza utekelezaji wa dira ya Maendeleo ya 2050 imefungua milango ya kidiplomasia ili kuwaalika wawekezaji kuwekeza hapa nchini.

“Kama serikali tumewahakikishia kuwa kupitia Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji tumewahakikishia kwamba watakapokuwa tayari tutawepeleka kwenye maeneo ya kimkakati ili kutekeleza miradi yao katika sekta za Utalii, Afya na Elimu.” Alisema.








 

Post a Comment

0 Comments