Na. Mwandishi Wetu.

Kwa mujibu wa taarifa kwa Umma iliyotolewa na kusainiwa na Mkurugenzi Mkuu wa TMDA, Imebainisha kuwa;
Lengo la Tuzo hizo ni kutambua mchango wa Waandishi wa habari na kuleta hamasa katika kuelimisha jamii kuhusu masuala ya udhibiti wa dawa, vifaa tiba, vitendanishi na bidhaa za tumbaku kupitia vyombo vya habari ili kulinda afya ya jamii.
"Kazi zinazolengwa ni zile zilizoripotiwa kupitia runinga (TV), Redio, Magazeti na mitandao ya kijamii kwa kipindi tajwa, ambapo baada ya kupokelewa zitashindanishwa na hatimaye kuwapata washindi watakaopewa tuzo.
"TMDA inawaalika waandishi kuwasilisha kazi zao ifikapo au kabla ya tarehe 18 Aprili, 2025 kupitia anuani ya barua pepe ya commpedtmda@gmail.com au kwa njia ya CD katika ofisi za TMDA zilizopo Dodoma, Dar es salaam, Mwanza, Arusha, Mbeya, Mtwara, Tabora na Geita." Imeeleza taarifa hiyo.
Aidha, tuzo hizo zimekuwa zikitolewa kila mwaka huku zikiongeza tija na ufanisi kwa Wanahabari nchini kuendelea kuandika na kuripoti habari juu ya Udhibiti wa Dawa.
0 Comments