Azitaka nchi za Afrika kuunganisha nguvu
Wajumbe wamsifu Rais Samia kwa kuwa kinara
Na John Mapepele- Addis Abbaba.
Waziri wa afya, Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema Afrika inatakiwa kuunganisha nguvu katika kuweka mikakati ya pamoja katika kupunguza vifo vya mama na mtoto ili kuondokana na changamoto hiyo.
Mhe. Mchengerwa ametoa kauli hiyo leo Februari 13, 2026 jijini Addis Abbaba nchinini Ethiopia kwenye mkutano wa Nchi zote za Umoja wa Afrika wakati anafungukua mkutano huo, akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Mhe. Mchengerwa amesema Umoja wan chi za Afrika umeipa Tanzania heshima kubwa ya kufungua mkutano huo kwa kutambua juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali ya Tanzania ikiongozwa na Rais, Samia Suluhu Hassan katika kupunguza kwa kasi vifo vya mama na mtoto wakati wa kujifungua.
“Ni ukweli usiopingika kuwa Rais Samia amefanya kazi kubwa sana katika eneo hili la kupunguza vifo vya mama na mtoto katika kipindi kifupi na kupata tuzo nyingi, na ndiyo sababu wameipatia nchi yetu hesghima ya kufungua mkutano huu mkubwa”.Amefafanua Mhe. Mchengerwa
Mkutano huu umehudhuliwa na takribani nchi zote za Afrika ambapo mawazari wa Afya wa nchi hizo wamepata fursa ya kufanya majadiliano ya namna bora ya kukabiliana na changamoto ya vifo vya mama na mtoto huku Tanzania ikipigiwa mfano wa kufanya vizuri katika eneo hili.
Aidha, wajumbe wameonyesha kuridhishwa na hatua zinazochukuliwa na nchi wanachama na kwamba kumekuwa na mafanikio yanayoonekana kupitia kampeni ijulikanayo kama CARMMA (2021- 20300 chini ya Umoja wa Nchi za Afrika inayolenga kupunguza vifo vya mama na mtoto.
Mkutano huu unafanyika jijini Addis Ababa nchini Ethiopia pembezoni mwa Mkutano wa 39 wa Wakuu wa Nchi wa Umoja wa Afrika unaofanyika kesho na kesho kutwa ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan anashiriki na amependekezwa kuwa kinara wa Umoja wa Afrika katika Masuala ya Afya ya Mama na Mtoto, uteuzi ambao unatarajiwa kupitishwa rasmi na Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali.


.jpeg)
.jpeg)

0 Comments