Na Mwandishi Wetu
Tume ya Ushindani (FCC) imesema kufuatia taarifa za kiintelijensia katika soko la Kariakoo ilifanya operesheni ya ukamataji wa vilainishi bandia vya magari vilivyokuwa na alama za biashara zinazomilikiwa bila ridhaa za wamiliki wa alama hizo.
Katika taarifa iliyotoelwa na Kitengo cha Mawasiliano na Mahusiano ya Umma
Tume ya Ushindani (FCC) imesema operesheni hiyo ilifanyika katika eneo la Kariakoo, Mtaa wa Udoe, Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam na kukamata madumu zaidi ya 5,000 yenye ujazo tofauti wa vilainishi yanashukiwa kuwa bandia,mashine tatu za uzalishaji/ujazaji upya pamoja na stika za chapa bandia
Bidhaa na vifaa vyote vilivyokamatwa vimehifadhiwa kama vielelezo, vikisubiri uthibitisho kutoka kwa wamiliki wa alama za bidhaa husika.
Kwa mujibu wa taarifa ilisema ukamataji wa vilainishi hivyo vya magari vinavyoshukiwa kuwa bandia ulifanyika kwa mujibu wa sheria
FCC inatoa rai kwa wafanyabiashara kutojihusisha na utengenezaji, usambazaji, au uuzaji wa bidhaa bandia ya aina yoyote ikiwemo vilainishi vya magari vina madhara makubwa ikiwemo kuharibu injini, kusababisha hasara ya kifedha, na kuhatarisha usalama.
Hata hivyo wafanyabiashara na umma kwa ujumla kufahamu kwamba bidhaa bandia huhatarisha usalama wa maisha, mali na afya za walaji na zina athari kubwa kwa biashara halali na uwekezaji
nchini kwani zinaleta ulingo usio sawa katika biashara .
FCC inawahimiza wananchi kutoa taarifa FCC kuhusu uwepo wa shughuli zinazohusiana na bidhaa bandia kupitia simu ya bure 0800 11 00 94 au info@fcc.go.tz kwa ajili ya kuchukua hatua stahiki kwa mujibu wa Sheria ya Alama za Bidhaa. Kwa pamoja tunaweza kuifanya Tanzania kuwa salama bila ya bidhaa bandia.

.jpeg)
0 Comments