About Me

header ads

FCC YAKUTANA NA TAFFA

Tume ya Ushindani (FCC) yakutana na Uongozi wa Chama cha Mawakala wa Mizigo Tanzania (TAFFA) ili kujadili mambo mbalimbali yanayohusu utekelezaji wa Sheria ya Alama za Bidhaa ikiwa ni pamoja na kuboresha na kutatua kero zinazoweza kujitokeza katika utekelezaji wa majukumu hayo.
Akizungumza wakati wa kufungua kikao hicho Mkurugenzi Mkuu wa FCC Bw. William Erio amesema kuwa kwa mwaka huu Tume itajikita katika utoaji wa elimu kwa wadau wa biashara na waingizaji wa bidhaa ili kupunguza changamoto zinazohusiana na masuala ya alama za bidhaa.

Kikao hiki ni muendelezo wa FCC kukutana na wadau wake na kujadili namna bora ya matumizi ya alama za bidhaa, kuweka mazingira wezeshi ya kibiashara na kushajiisha ushindani katika soko.
Kwa upande wake akizungumza kwa niaba ya TAFFA Bw. Waheed Saudin, Makam wa Rais wa TAFFA ameishukuru FCC kwa kuwa na desturi ya kuwaita wadau wake, kukaa pamoja na kujadili namna mbalimbali za kuweka mazingira wezeshi ya kibiashara ikiwa ni pamoja na kutatua changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika mazingira ya kibiashara.

Kikao hiki kimefanyika tarehe 17 Januari, 2025 katika ofisi ya FCC Dar es Salaam.












 

Post a Comment

0 Comments