KANISA la Anglikan Catholic church Jimbo la Tanzania limewahamasisha wananchi wa Mkoa wa Dodoma kushiriki kikamilifu katika mchakato wa uwandikishaji kwenye daftari la kudumu la wapiga kura linalotaraji kuanza Oktoba 25 mpaka mpaka Novemba 1 mwaka huu mkoani humo.
Askofu Mkuu wa Anglikan Catholic church Jimbo la Tanzania,Dk. Elibariki Philip Kutta ametoa hamasa hiyo kijijini Mlali wilayani Kongwa mkoani Dodoma muda mfupi uliopita baada ya kusimikwa kwa Askofu Mkuu wa kwanza wa Kanisa hilo Nchini
Amewahimiza wananchi wa Mkoa wa Dodoma kuwa wakati ukifika wakajiandikishe kwenye daftari hilo ili watumie fursa hiyo kuwachagua Viongozi wenye hofu ya Mungu katika kuwaletea maendeleo Wananchi
Aidha Askofu Kutta amesema wananchi wakiwachagua Viongozi wenye hofu ya Mungu ni rahisi Viongozi hao kuwaletea maendeleleo.
0 Comments