Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amevitaka vyuo vikuu nchini kutenga Fedha kwa ajili ya tafiti zitakazo saidia kutatua changamoto za jamii ya Tanzania.
Ameyasema hayo mkoani leo Novemba 22, 2023 Morogoro wakati akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa Baraza la 23 la wahitimu wa Chuo Kikuu Mzumbe.
Amesema Serikali tayari imeandaa mazingira wezeshi ya kuongeza nguvu katika matumizi ya Tehama , ili kuendana na kasi ya utandawazi
Aidha Prof. Mkenda ameongeza kwa mwaka wa fedha 2022/23 Serikali imetenga kiasi cha sh millioni 500 kwa Chuo Kikuu Mzumbe ili kuboresha miundombinu ya Chuo hicho.
Kwa upande wake Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. Williamu Mwegoha
ameeleza mafanikio mbalimbali ya Chuo hicho ikiwemo kukamilisha ujenzi wa hostel ambazo zitabeba zaidi ya wanafunzi 1026, kuongezeka kwa udahiri wa wanafunzi na kufikia asilimia 17.3%.
Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Prof. Elisante Ole Gabriel, akizungumza wati wa Mkutano Mkuu wa Baraza la 23 la wahitimu wa Chuo Kikuu Mzumbe.
Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. Saida Yahya Othman (kulia) akiteta jambo na Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. William Mwegoha.Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akisoma hotuba yake wakati wa Mkutano Mkuu wa Baraza la 23 la wahitimu wa Chuo Kikuu Mzumbe.
Sehemu ya watumishi wa chuo hicho.
Sehemu ya watumishi wa chuo hicho. (PICHA ZOTE NA EMMANUEL MASSAKA,MICHUIZI TV)
0 Comments