Na Mwandishi wetu- Kigoma
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Jerry Silaa amewataka wananchi kote Nchini ambao zoezi la urasimishaji Ardhi linaendelea katika maeneo yao kuhakikisha wanalipia, wanapimiwa na baadae kufuatilia hati zao ili ardhi wanayomiliki iweze kupanda thamani.
Waziri Silaa alisema utoaji huduma kwa njia ya Kliniki unarahisisha kazi kwa Wananchi kwani unawaondolea usumbufu lakini pia unafanyika hadharani na mwananchi akifika anapatiwa huduma zote kesho yake anakuja kuchukua hati yake.
Waziri Silaa alisema hayo jana alipofika katika Kijiji cha Msimba Kata ya Mungunya kilichopo nje Kidogo ya Manispaa ya Kigoma kwa lengo la kugawa hati kwa wakazi hao ambao tayari wamekamilisha taratibu za urasimishaji.
Aidha Waziri Silaa alitoa maelekezo kwa Kamishna Msaidizi wa Ardhi Mkoani Kigoma kuhakikisha anafanya kazi hiyo kama ilivyo kwa maeneo mengine ili mwananchi akifika katika eneo hilo apatiwe hati yake nakuondoka.
‘’Ninyi wenyewe mnaona kuwa si kila mwananchi anaweza kuingia katika ofisi za serikali mwingine akiingia ndani ya eneo la serikali haimwingii akilini kwani kuna wakati anaona anaonewa anaona kuna vyumba vingi vinamchanganya.’’Alisema Waziri Silaa.
Waziri Silaa aliwataja watendaji kuwa waadilifu na kubainisha pia kuwa baadhi yao sio waadilifu hivyo kutajia wananchi viwango vya malipo ambavyo uchangia wananchi hao kushindwa kufuatilia huduma ya sekta ya ardhi na kuiongeza kuwa Serikali ya Rais Samia imepunguza gaharama za kulipia hati kwa 50%.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Bw.Salum Kalli amewambia wananchi waliofika katika Kliniki hiyo kutambua kuwa kumilki ardhi yenye hati kuna thamani kubwa kiuchumi tofauti na wale wanaomilki ardhi bila kuirasimisha.
Kiongozi huyo wa Wilaya alisema kuwa na hati ndiyo maisha kwani ukishakuwa na hati wewe ni tajiri kwa kuwa unakopeshaka na ukiwa na hati miliki unalinga na kubeza.
‘’Hati ni pesa, hati ni nyumba, hati ni maendeleo, hati ni Maisha ukienda Benki kama hutaki kuonga unamwonesha Meneja unasema unaona hii hati niliyonayo tayari unakuwa na pesa yenye thamani ya Milioni 30.’’ ’’Alisema kiongozi huyo wa Wilaya.
Mkuu huyo wa Wilaya aliongeza kuwa unaweza ukawa na ardhi ndogo yenye hati ikawa na thamani kubwa kuliko ya mtu anayemiliki mashamaba makubwa ambayo hayana hati kwani anayemiliki ardhi bila kuirasimisha hawezi kutumia ardhi hiyo kama dhamana ya kujipatia mkopo Benki.
Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa muda sasa imekuwa ikiendesha zoezi Urasimishaji kote Nchini kupitia Kliniki za Ardhi kila Mkoa kwa lengo la kurasimisha ardhi na makazi lakini pia kutumia fursa hiyo kutatua Migogoro ya Ardhi kwa wananchi.Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendekeo ya Makazi Jerry Silaa akiongea na Wananchi wa Kijiji cha Msimba Kata ya Mungunya kilichopo nje Kidogo ya Manispaa ya Kigoma wakati wa zoezi la ugawaji hati kwa wanachi walioshiriki zoezi la urasimishaji unaoendelea Mkoani Kigoma jana. Watalaamu wa Sekta ya Ardhi kutoka Manispaa ya Kigoma wakiendelea na zoezi la utoaji hati kwa Wananchi wa Kijiji cha Msimba Kata ya Mungunya kilichopo nje Kidogo ya Manispaa ya Kigoma wakati wa zoezi la ugawaji hati kwa wanachi walioshiriki zoezi la urasimishaji unaoendelea Mkoani Kigoma jana. Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendekeo ya Makazi Jerry Silaa akikabidhi hati kwa Bi. Furaha Kapipi Bukulu mkazi wa Kijiji cha Msimba Kata ya Mungunya kilichopo nje Kidogo ya Manispaa ya Kigoma wakati wa zoezi la ugawaji hati kwa wanachi walioshiriki zoezi la urasimishaji unaoendelea Mkoani. Kigoma jana. Wananchi wa Kijiji cha Msimba Kata ya Mungunya kilichopo nje Kidogo ya Manispaa ya Kigoma wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Ardhi Jerry Silaa mara baada kupata hati zao wakati wa zoezi la ugawaji hati kwa wanachi walioshiriki zoezi la urasimishaji unaoendelea Mkoani Kigoma jana.
0 Comments