Mke wa Rais wa Zanzibar, Msarifu na Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini ya Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation Mhe.Mama Mariam Mwinyi amesema juhudi za Serikali ya awamu ya nane inayoongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi katika kukabiliana na vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia ikiwemo kuanzishwa kwa Mahakama Maalumu za kushughulikia mashauri ya udhalilishaji wa kijinsia, kuondoshwa dhamana kwa watuhumiwa wa vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia na kuharakisha muda wa kusikiliza kesi za udhalilishaji na hukumu.
Mama Mariam Mwinyi amesema hayo akiwasilisha mchango wake katika mkutano wa Viongozi Wanawake ulioandaliwa na Jumuiya ya Madola ukumbi wa Marlborough House, London Uingereza tarehe 15 Novemba 2023.
Aidha, Mama Mariam Mwinyi ameeleza malengo na uzoefu wa Taasisi ya ZMBF katika kuchangia juhudi za Serikali kuinua ustawi wa maisha kwa Wanawake, Vijana na Watoto ikiwemo uwezeshaji wa Wanawake kiuchumi hususani wakulima wa Mwani, kuimarisha afya ya Mama na mtoto, kuanzisha program ya kusaidia upatikanaji wa Taulo za kike.
0 Comments