Na Dotto Mwaibale, Arusha
UMOJA wa Wanamuziki Tanzania (TAMUFO) umeiomba Serikali
kuendelea kutoa elimu kwa wananchi ili waweze kujua faida ya mkataba wa bandari ya Dar es Salaam dhidi ya Kampuni ya DP World ya Dubai.
Ombi hilo limetolewa na Katibu Mkuu wa TAMUFO,
Stellah Joel wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa jana huku
akielezea umuhimu wa uendelezaji wa bandari yetu ya Dar es Salaam kupitia mkataba huo.
“Nimekuwa nikifuatilia kwa karibu kuhusu
uwekezaji wa uendeshaji wa bandari naona changamoto kubwa ni wananchi kutoa
elewa vizuri juu ya uwekezaji huu ambao utaongeza pato la taifa,” alisema Joel.
Alisema watanzania siku zote ni waelewa na kuwa
nchi yetu imekuwa na makampuni mengi ambayo yamewekeza katika maeneo mengi
jambo ambalo ni la msingi katika kuinua uchumi.
Alisema tayari Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania limekwisha ridhia mkataba huo baada ya kujiridhisha kuwa utakuwa na
tija hivyo kazi kubwa iliyopo ni kwa wanasheria na wataalamu mbalimbali
wakiwemo waandishi wa habari kutoka na kwenda kutoa elimu kwa wananchi kuhusu
faida ambayo nchi itaipata kupitia uwekezaji huo.
Mlezi wa TAMFO, Dk.Frank Richard alisema Serikali iliridhia mkataba huo baada ya kupitia mawasilisho ya kampuni hiyo pamoja na sifa zao kimataifa na kuamua kuanzisha majadiliano na kampuni ya DP World kwa kuzingatia uzoefu wake katika uendeshaji wa shughuli za bandari barani Afrika, Asia, Ulaya na Amerika ya Kaskazini na Kusini.
Alisema suala hili lisitugawe watanzania kwa
namna moja ama nyingine kwani Rais Dk. Samia Suluhu Hassan hawezi kuiuza
bandari ambayo ndio chanzo kikubwa cha mapato ya nchi kwani ana lengo zuri la
kuongeza mapato kupitia uwekezaji huo mkubwa wenye tija.
0 Comments