About Me

header ads

SUA YAPONGEZWA KWA MCHANGO WAKE KATIKA UHIFADHI NA UTALII NCHINI.

 

Na: Calvin Gwabara- Mikumi.

Wahifadhi katika hifadhi ya Taifa ya Mikumi Mkoani Morogoro wanajivunia matunda ya kazi nzuri inayofanywa na Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA ya kuzalisha Wahifadhi bora nchini kupitia
mafunzo kwa vitendo na Wakufunzo wake wabobevu.

Hayo yamebainishwa na askari uhifadhi daraja la kwanza katika hifadhi hiyo Mhifadhi Nicas Nguma wakati akiongea na SUAMEDIA juu ya mchango wa SUA na ushirikiano uliopo kati ya TANAPA na Chuo hicho katika kusaidia mafunzo kwa vitendo ya wanafunzi wake.

‘’Ukifanya tathimini ya kina kwenye hifadhi zetu utakuta takribani asilimia 75 au zaidi ya Wahifadhi wetu ni Wanafunzi ambao wametoka Chuo Kikuu cha Sokoine n ahata sasa wengine wengine ambao wameajiriwa tayari wapo masomoni SUA, Kwahiyo Chuo hiki kina mchango mkubwa sana kwenye uhifadhi nah ii inatokana na ubora wao katika kazi kupitia mafunzo kutoka
SUA‘’ Alifafanua Mhifadhi Nguma.

Aidha amesema kuwa wamekuwa wakipokea wanafunzi wa ngazi mbalimbali kutoka SUA kwaajili ya mafunzo kwa vitendo kila mwaka na kubainisha kuwa ni wanafunzi wazuri ambao watasaidia nchi katika
kutunza maliasili za taifa kwani hawapati shida wanapokuwa wanawafundisha uhifadhi kwa vitendo hifadhini humo.

Kwa upande wao baadhi ya Wanafunzi wa mwaka wa kwanza wanaosoma Shahada ya Uzimamizi wa Wanyamapori kutoka Ndaki ya Misitu Wanyamapori na Utalii ya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo wamesema katika kipindi kifupi toka waanze masomo wameweza kufahamu mambo
mengi ambayo yanawafanya kupenda zaidi fani ya Uhifadhi.

Akizunguzia mafunzo kwa vitendo wanayoyapata kwenye Hifadhi ya mikumi Mwanafunzi wa mwaka wa kwanza Yassin Jafari amesema baada ya nadharia za darasani chuoni sasa wamekuja kufanya kwa vitendo huku akijivunia mbinu ya kutambua falme za wanyama na aina zake kwa ishara ikiwemo kupitia kuangalia nyayo walizokanyaga na kinyesi.

Kwa upande wake Ester Tairo amesema mahusiano mazuri kati ya Chuo na TANAPA kunawawezesha kupokelewa vizuri na kupata ushirikiano mkubwa kutoka kwa wahifadhi katika hifadhi hiyo ya Mikumi kwa kushirikiana na walimu wasimamizi kutoka SUA na hivyo kufurahia mafunzo hayo wakati wote.

‘’Sisi hapa ni mwaka wa kwanza wa Shahada ya Uzimamizi wa Wanyamapori tumesoma kidogo darasani lakini sasa tumeletwa Hifadhini kwaajili ya kuona na kutenda vile tulivyofundishwa kwa vitendo kitu
ambacho sio rahisi kufanywa na vyuo vingine nchini na tumepitia kwenye mafunzo yote ya Uhifadhi, Utambuzi wa Mimea,Aina za wanyama na tabia zao pamoja na Ukarimu kwa wageni kiukweli tumeiva kwa muda mfupi tu hapa tukiwa mwaka wa kwanza‘’ Alieleza Ester.

Wanafunzi hao wa mwaka wa kwanza wapo kwenye mafunzo kwa vitendo kwenye hifadhi mbalimbali nchini ikiwemo Mikumi,Tarangire na nyingine wakijivunia mafunzo hayo huku wengine ambao hawakuwahi kuwaona wanyama hao uso kwa uso kwa mara ya kwanza.Askari Uhifadhi daraja la kwanza katika Hifadhi ya Taifa ya Mikumi Nicas Nguma akizungumza na SUAMEDIA hifadhini hapo.
Mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Shahada ya Uzimamizi wa Wanyamapori kutoka Ndaki ya Misitu Wanyamapori na Utalii ya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo Yassin Jafari (wa pili kulia) akieleza anavyonufaika na mafunzo kwa vitendo huku wanafunzi akicheza mchezo wa drafti na wanafunzi wenzake wakati wa mapumziko kambinu hapo.

Mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Shahada ya Usimamizi wa Wanyamapori kutoka Ndaki ya Misitu Wanyamapori na Utalii ya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo Ester Tairo akieleza yale wanayojifunza kwenye Hifadhi hiyo na faida za kusoma SUA.

Profesa mbobevu wa Ikolojia kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo Prof. Pantaleo Munishi akiteta jambo na kutoa maelekezo kwa wanafunzi hao kabla ya kuelekea porini kwenye hifadhi ya Taifa ya Mikumi Mkoani Morogoro.

Rasi wa Ndaki ya Misitu Wanyamapori na Utalii katika ChUO Kikuu cha Sokoine cha Kilimo Dkt.Agnes Sirima akizungumza na wanafunzi hao wakati wa mapumziko wakiwa kwenye Hifadhi hiyo ya Taifa ya
Mikumi.

Post a Comment

0 Comments