SEKTA ya utalii imepata ahueni ya kipekee katika kuhudumia watalii baada ya kampuni ya Tempo Africa kuanzisha mfumo wa kuhudumia watalii wa ndani na nje ya nchi kwa kutumia application maalumu itakayowawezesha watalii kupata huduma tofauti kwa pamoja.
Mfumo huo mpya unawawezesha watalii kuagiza na kupata bidhaa na huduma kupitia application hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Mei 30,2023 Jijini Dar es Salaam kuhusiana na huduma hiyo mpya, Mkurugenzi Mtendaji wa Tempo Africa, Pendo Lema, amesema, kufuatia pengo la kuhudumia wageni na changamoto zinazohusiana na huduma mbalimbali wanazopata katika sekta hiyo, kampuni hiyo imeamua kuja na ufumbuzi wake kupitia huduma hiyo mpya.
"Ububunifu wetu umejikita zaidi katika kuboresha huduma bora za kukodisha nyumba, usafiri wa aina mbalimbali, huduma ya tiketi za ndege na huduma zingine za utalii kwa ujumla," alisema.
Ameongeza, kwa kusema kuwa kampuni ya Tempo Afrika ambao ni watoa huduma ya utalii inayoaminika katika kutoa huduma zake malimbali, "Tunawapa wateja wetu mikataba bora na yenye masharti nafuu na pia watapata huduma kutoka kwa timu yetu yenye wafanyikazi wenye uzoefu wa hali ya juu”.
Amewahakikishia watalii wanaokuja nchini kuwa watapata huduma nzuri, salama na za uhakika zikiwemo zile za kutembelea maeneo ya utalii ya kihistoria hapa nchini Tanzania, kupata usafiri bora kwa gharama nafuu na kupitia huduma za magari ya Tempo, huduma ya kuhifadhiwa vyumba vya malazi kwenye hoteli, huduma ya tiketi za ndege, mawasiliano na makampuni mbalimbali ya utalii na waongoza utalii wenye weledi, yote hayo kwa gharama nafuu huku akibainisha kuwa huduma zote hizi zinapatikana kwenye application ya tovuti ya Tempo.
Kwa upande wa application ya simu ya mkononi, amesema kwa sasa watumiaji wanaweza kupata huduma kuhusu nyumba za kupanga, hoteli na lodge mbalimbali lakini wana mpango wa kuhakikisha huduma zote zinapatikana kwenye app ya tovuti na app ya simu za mkononi.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji huyo, hatua hiyo ya ubora wa huduma hizo inalenga katika kuchangia juhudi za serikali katika kutangaza utalii wa Tanzania kama miongoni vituo muhimu vya utalii na vyeye ubora.
“Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa mstari wa mbele katika kutangaza utalii kupitia Filamu ya Royal Tour ambayo sasa ni maarufu katika nchi nyingi; tunataka watalii hawa wawe na wakati mzuri kwa kupata huduma nzuri na zenye unafuu kwa rahisi kupitia huduma za simu zao za viganjani wakiwa majumbani mwao”, amesema.
Amesema kampuni yake iko tayari kushirikiana na Wizara ya Maliasili na Utalii katika kuhakikisha watalii wanapata huduma ziakazowafanya waikumbuke Tanzania na kuifanya kama kituo cha bora cha utalii watakachokitembelea mara kwa mara.
Aidha ametoa wito kwa Watanzania pia kutumia vyema huduma hiyo mpya kupata huduma na bidhaa mbalimbali za utalii ambazo ni pamoja na kupangisha nyumba za kuishi jambo ambalo kwa sasa ni kero kubwa kwa Watanzania wengi.
Alisema Tempo Africa ilianzishwa mwaka 2021 na imesajiliwa nchini Tanzania.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Tempo Africa, Pendo Lema (katikati) akizunguza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa application maalumu kwa ajili ya simu za mkononi na tovuti inayohusinana na taarifa za utalii Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja Biashara wa kampuni hiyo, Taddei Swain na Meneja Mahusiano Millian Lema.
0 Comments