About Me

header ads

Waandishi wanne wang'aa tuzo za TMDA


NA EMMANUEL MASSAKA  

Mwandishi wa habari wa Dailynews Digital Aveline Kitomary ameibuka mshindi wa jumla wa uandishi wa habari za dawa,vifaa tiba na Vitendanishi tuzo zilizotilewa na Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA)

Tuzo hizo zimetolewa Wilayani Babati, Mkoani Manyara wakati wa kikao kazi cha Wahariri na Waandishi wa habari wa kanda ya Kaskazini inayojumuisha mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Manyara.

Katika hafla hizo Aveline amechukua pia tuzo nyingine ya uandishi upande wa kundi la magazeti hii ikiwa ni mara ya tatu kutwaa tuzo hizo.

Akizungumza wakati alipopoke tuzo hizo Aveline amesema kuwa siri ya mafanikio hayo ni kujituma na kufanya kazi kwa bidii hasa katika kuandika habari za kijamii.

"Katika kipindi cha mwaka mmoja  habari na makala za dawa,vifaa tiba na vitendanishi takribani 19 na hii imekuwa inahitaji bidii kwasababu kuna makala zingine nimefatilia muda mrefu tu.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa TMDA ,Yona Mwalu amesema jumla ya kazi 26 ziliwasilishwa ambapo ushindani wa kazi ulikuwa mkubwa.

"Tutaendelea kutoa tuzo na kuongeza zawadi kila mwaka tunataka waandishi wa nchi nzima washiriki katika tuzo hizi hivyo kwa mwaka ujao tunategemea ushindani zaidi.,"amesema.

Amesema tuzo hizo zinavipengele vitano ambavyo ni kundi la televisheni, redio,vyomba vya habari vya mitandaoni na mshindi wa jumla.

Aidha katika kila kundi mshindi amepata fedha taslimu kiasi cha Sh milioni moja na cheti.


Post a Comment

0 Comments