SHIRIKA lisilo la Kiserikali la Kilimanjaro Dialogue Institute (KDI) lenye makao yake jijini Dar es salaam linalofanya shughuli za kukuza na kudumisha amani na maridhiano,limefuturisha waumini wa madhebu tofauti katika mwezi huu wa mfungo wa Ramadhan.
Katika futari hiyo Mgeni rasmi alikuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT) Sheikh, Daktari Alhad Musa Salum ambaye aliongozwa wageni waalikwa mbalimbali.
Wakati wa chakula, wageni walikuwa na nafasi ya kushiriki katika mazungumzo ya kupitia miongozo na kushiriki katika tafakari juu ya umuhimu wa Ramadhani na Kwaresma katika imani zao.
Tukio hilo lililenga kukuza uelewa, heshima, na mshikamano kati ya watu wa asili tofauti za kidini, likitilia mkazo umuhimu wa upendo na umoja katika jamii yenye watu wa imani tofauti.
Akizungumza katika tukio hilo, Mwenyekiti wa taasisi hiyo Ibrahim Yunus amegusia umuhimu wa kudumisha amani katika jamii ambapo amesema kila mmoja wetu anashiriki kikamilifu katika kuhakikisha amani iliyopo nchini inaendelea kudumishwa.
0 Comments