Na Mwandishi Wetu
Na Mwandishi Wetu
MJUMBE wa Kamati ya Utekelezaji ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Taifa, Mariam Abdallah Ibrahim, amefanya ziara ya kikazi katika Wilaya ya Gairo,mkoani Morogoro, kwa lengo la kukagua shughuli za maendeleo zinazotekelezwa na wanawake kupitia umoja huo.
Katika ziara hiyo, Mariam Ibrahim ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Pwani ametembelea na kukagua vikundi vya wajasiriamali , huku akiwapongeza kwa juhudi zao za kujiongezea kipato na kuchangia maendeleo ya familia pamoja na taifa.
Akizungumza na wananchi na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) amewashukuru wakazi wa Mkoa wa Morogoro kwa kukichagua Chama Cha Mapinduzi katika Uchaguzi Mkuu kwa kumpatia kura nyingi Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na kuwachagua wabunge na madiwani wa chama hicho.
Pia amewahimiza wanawake kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi za uongozi ndani ya CCM, akieleza kuwa ushiriki wao katika nafasi za maamuzi ni muhimu katika kuimarisha maendeleo na kuendelea kutetea maslahi ya wanawake na jamii kwa ujumla.
Mjumbe huyo wa Kamati ya utekelezaji UWT Taifa amefanya ziara hiyo ikiwa ni sehemu ya juhudi za UWT Taifa za kufuatilia utekelezaji wa shughuli za jumuiya hiyo, kuhamasisha maendeleo ya wanawake, na kuimarisha ushiriki wao katika shughuli za kisiasa, kijamii na kiuchumi.


.jpeg)










.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)


0 Comments