About Me

header ads

JUMUIYA YA WAZAZI CCM MKOA WA DAR ES SALAAM YAADHIMISHA MIAKA 49 YA CCM KWA KAZI ZA KIJAMII TEMEKE

 

Dar es Salaam 02 Februari, 2026

Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam leo tarehe 02 Februari, 2026, imeungana na wanaCCM na wananchi kwa ujumla kuadhimisha kilele cha miaka 49 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi, kwa kufanya shughuli mbalimbali za kijamii katika Wilaya ya Temeke.

Katika maadhimisho hayo ya kimkoa, Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa DSM ilitembelea Hospitali ya Round Table Mbagala, wodi ya wazazi, na kutoa msaada wa vifaa vya kujifungulia (delivery kits) kwa akina mama wajawazito 22.

Aidha, msaada huo uliambatana na ugawaji wa pampers, sabuni pamoja na maji ya kunywa, ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono afya ya mama na mtoto.

Kadhalika, Jumuiya ilitembelea Kituo cha Hiari Orphanage Center, ambapo ilikabidhi mahitaji maalum kwa ajili ya kuwasaidia watoto wanaolelewa katika kituo hicho, ikiwa ni ishara ya mshikamano na upendo kwa makundi yenye uhitaji maalum.

Kwa sasa, viongozi na wajumbe wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Dar es Salaam wamekutana katika ukumbi wa Ikweta Grill – Mtoni kwa ajili ya kikao cha ndani, ambapo pia kutatolewa viti mwendo (wheelchairs) vinne kwa watoto wenye uhitaji maalum.

Jumuiya ya Wazazi inaendelea kusisitiza dhamira yake ya kushiriki kikamilifu katika kujenga jamii bora, yenye mshikamano na maendeleo kwa maslahi mapana ya Taifa.
Happy 49th Birthday CCM!

Wazazi tupo mtaani kujenga jamii bora kwa maslahi ya Taifa.
Imetolewa na:

Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Dar es Salaam.













Post a Comment

0 Comments