Na Mwandishi wetu ,Dar es Salaam
WADAU zaidi ya 100 kutoka taasisi za serikali, mamlaka za bandari na usafiri, sekta binafsi ya usafirishaji, waagizaji, wauzaji nje na wamiliki wa mizigo wamekutana jijini Dar es Salaam kujadili ufanisi wa bandari na uendelevu wa uendeshaji wake kupitia ushirikiano wa sekta ya Umma na binafsi (PPP).
Mkutano huo wa majadiliano ya pamoja kati ya sekta ya umma na binafsi umelenga kubaini changamoto za biashara na usafirishaji katika bandari za Tanzania, kujadili suluhisho za vitendo kupitia ushirikiano wa sekta hizo mbili, pamoja na kuangalia namna ya kuwezesha biashara na kuendeleza miundombinu ya bandari.
Mada kuu ya mjadala huo ilikuwa “Kuendesha Operesheni Endelevu za Bandari Kupitia Ushirikiano wa Umma na Binafsi.”
Kwa upande wake, Kanali mstaafu Joseph Simbakalia, aliyekuwa mchokoza mada kuhusu matumizi ya PPP katika maendeleo ya miundombinu ya biashara, alisema ni muhimu kwa sekta za kimkakati kumilikiwa, kudhibitiwa na kuendeshwa na Watanzania.

0 Comments