📍 Dar es Salaam
Kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Ushindani Duniani Tume ya Ushindani (FCC) imekukutana na wadau wote wanaohusika na utoaji wa mizigo bandarini kupitia chama chao cha Mawakala wa Forodha Tanzania (TAFFA) ili kuwapa elimu na kuwafahamisha kuwa FCC imeingia katika mfumo rasmi wa ukaguzi bidhaa wa pamoja yaani Tanzania Other Government Agencies (TANOGA) ili kurahisisha ukaguzi wa bidhaa bandia ambapo kupitia mfumo huu ukaguzi unafanyika kwa pamoja na mamlaka zingine za udhibiti za Serikali.
Nae Makamu wa Rais wa Chama cha Mawakala wa Forodha Tanzania (TAFFA) Bw. Wahid Sahdin amesema kuwa TAFFA itaendelea kuipa Tume ushirikiano katika kupambana na bidhaa bandia zinazoingia nchini kwa njia mbalimbali ikiwemo bandari.
Tume ya Ushindani (FCC) imekuwa na kawaida ya kukutana na wadau wake mara kwa mara ikiwa ni muendelezo wa zoezi la utekelezaji wa mpango wa elimu kwa Umma unaorahisisha utekelezaji wa Sheria inazozisimamia.
Semina hiyo ilitolewa Disemba 2, 2025 Katika ukumbi wa Mikutano wa Serengeti ulio katika ofisi za FCC, jijini Dar es Salaam.

0 Comments