
Prof. Pallangyo ametoa pongezi hizo alipotembelea banda la PPAA katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayoendelea Jijini Dar es Salaam.
Akiongea kwa niaba ya Katibu Mtendaji wa PPAA, Bw. James Sando, Afisa Mwandamizi wa Mamlaka ya Rufani, Bw. Stanley Jackson amesema kuwa Mamlaka ya Rufani imefanya mapinduzi makubwa ya teknolojia kwa kujenga Moduli ya kupokea na kushughulikia malalamiko na rufaa kupitia mfumo wa NesT ambapo moduli hiyo imerahisisha zoezi la kuwasilisha malalamiko na rufaa kwa wazabuni na Taasisi Nunuzi.
“Awali kabla ya ujenzi wa moduli, wazabuni walikuwa wanalazimika kufika katika ofisi za PPAA kuwasilisha malalamiko yao, ila sasa baada ya kujengwa kwa moduli mzabuni anawasilisha malalamiko na rufaa kieletroniki jambo linalo rahisisha na kuokoa muda na gharama kwa wazabuni na Taasisi Nunuzi,” amesema Bw. Jackson
Mwezi Februari, 2025 Serikali kupitia Wizara ya Fedha, ilizindua rasmi matumizi ya Moduli ya kupokea na kushughulikia malalamiko na rufaa katika Mfumo wa Ununuzi wa Umma kwa njia ya Kieletroniki (NeST) Jijini Mwanza wakati wa mafunzo ya moduli ya kupokea na kushughulikia malalamiko na rufaa (Complaint and Appeal Management Module) katika Mfumo wa NeST.
Hadi sasa PPAA imefanikiwa kutoa mafunzo kuhusu matumizi ya Moduli ya kuwasilisha na kushughulikia malalamiko na rufaa kwa njia ya kieletroniki katika kanda ya Pwani, ya Ziwa, Kaskazini, Nyanda za Juu Kusini na Kanda ya Kati zimepatiwa mafunzo. Aidha, katika mafunzo hayo PPAA imefanikiwa kutoa elimu kwa wazabuni 873 na wakuu wa idara/vitengo vya ununuzi na sheria wapatao 1,588 kutoka katika taasisi nunuzi 500.
Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Prof. William Pallangyo akipata maelezo kuhusu matumizi ya Moduli ya kupokea na kushughulikia Malalamiko na Rufaa katika mfumo wa NeST kutoka kwa Afisa Mwandamizi wa PPAA, Bw. Stanley Jackson wakati wa Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayoendelea Jijini Dar es Salaam
Baadhi ya wadau waliotembelea banda la PPAA kupata elimu ya huduma mbalimbali zinazotolewa na PPAA walipotembelea banda la PPAA katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayoendelea Jijini Dar es Salaam

.jpeg)
0 Comments