About Me

header ads

WASHIRIKI 1500 KUTOKA MATAIFA MBALIMBALI KUSHIRIKI KONGAMANO LA KILIMO NA LISHE

 

Na Mwandishi Wetu,Michuzi TV

WATALAAM zaidi 1500 wawekimo Wanasayansi, watunga sera kutoka sehemu mbalimbali duniani wanatarajiwa kushiriki Kongamano la Kimataifa la Kilimo na Lishe linalotarajia nchini Tanzania.
Akizungumza leo Juni 22,2025 jijini Dar es SalaamNaibu Makamu Mkuu wa SUA anayesimamia Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaalamu, Prof. Maulid Mwatawala, alisema kongamano hilo limeandaliwa kwa ushirikiano kati ya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) na Shule ya Lishe na Tiba za Magonjwa ya Kitropiki ya London (LSHTM).

Amesema katika kongamano hilo washiriki watajadili namna ya kuimarisha sekta ya kilimo na lishe duniani na kwamba limekuja wakati muafaka, kwani Serikali chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imejipanga kuboresha sekta ya kilimo na kuhakikisha wananchi wanakuwa na lishe bora.
Awali  Mwenyekiti Mwenza wa Kongamano hilo kutoka SUA, Prof. Joyce Kinabo, ameeleza kongamano hilo linafanyika wakati dunia ikikabiliwa na changamoto kubwa ikiwemo ya mabadiliko ya tabianchi, upungufu wa chakula, na utapiamlo. 

“Jambo la kushangaza ni kwamba licha ya Tanzania kuwa na mikoa inayozalisha chakula kwa wingi, bado kuna maeneo yanayokumbwa na utapiamlo au uzito kupita kiasi.”

Kwa upande wake Profesa Suneetha Kadiyala, mtaalamu wa kimataifa wa lishe kutoka LSHTM amesema kongamano hilo linatarajiwa kutoa mapendekezo ya kisera na kitaalamu yatakayosaidia mataifa wanachama kupambana na changamoto zinazoikumba sekta ya chakula na lishe, hasa katika kipindi hiki cha mabadiliko ya tabianchi na ongezeko la idadi ya watu.

Pia amesema  kongamano hilo linaunganisha nia ya kisiasa, uongozi wa kikanda na jamii ya kimataifa katika kuboresha mifumo ya chakula duniani.”Tangu kuanzishwa kwake mwaka 2016, jukwaa hili limekuwa likiwakutanisha wadau mbalimbali na limechangia kwa kiasi kikubwa kusaidia watunga sera kuboresha hali ya lishe.”


Sehemu ya waandishi wa habari wakiwa kwenye mkutano huo ulifanyika leo Juni 22,2025 jijini Dar es Salaam. (PICHA ZOTE NA EMMANUEL MASSSAKA, MICHUZI TV)

 

Post a Comment

0 Comments