About Me

header ads

TMDA YASHINDA TUZO PRST YA UMAHIRI WA KUTOAJI ELIMU KWA JAMII

 



Mkurugenzi wa udhibiti wa Dawa, Dkt. Yonah Mwalwisi (katikati) na  Meneja Mawasiliano na Elimu kwa Umma Gaudensia Simwanza,  wakiwa na tuzo hiyo. Kulia aliyekadhi tuzo hiyo Bw. Karim Meshaki, Mwenyekiti wa TAGCO

MAMLAKA ya Dawa na vifaa tiba nchini (TMDA ) kupitia kitengo cha Mawasiliano na Elimu kwa Umma imeshinda tuzo ya Umahiri katika Kampeni Bora ya utoaji Elimu kwa Jamii 2024 ikishinda kwa mara ya kwanza kipengele hicho.

Tuzo za kipekee za umahiri zimetolewa na Chama cha Maafisa Uhusiano na Mawasiliano Tanzania (PRST) hafla iliyofanyika Usiku wa tarehe 29 Machi, 2025 katika ukumbi wa Millenium Tower, Dar Es Salaam.

Aidha, katika tukio hilo tuzo hiyo imepokelewa na Mkurugenzi wa Udhibiti wa Dawa kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu, Dkt. Yonah Mwalwisi, na Gaudensia Simwanza, Meneja Mawasiliano na Elimu kwa Umma.

Tuzo waliokabidhiwa

Ushindi huo umetokana na mchango mkubwa unaotolewa na kitengo hicho cha Mawasiliano na Elimu kwa Umma kwa Jamii na vyombo vya habari mbalimbali nchini.

Katika tuzo hizo za PRST, TMDA imeweza kung'ara pia kwa Mwaka jana kwa kutwaa tuzo ya Taasisi yenye mahusiano mazuri na vyombo vya habari 2023.

Aidha , katika hafla hiyo Taasisi na Masharika mbalimbali yameshiriki katika mashindano hayo ya tuzo katika vipengele tofauti.

TMDA ilianzishwa mwaka 2003, hadi sasa ina miaka zaidi ya 20 ikiwa na majukumu ya kulinda afya ya jamii huku ikiwa na ofisi zake katika Kanda mbalimbali nchini sambamba na kuwa na maabara zenye kuhakikisha ubora, usalama na ufanisi wa vifaa tiba na dawa.



Sehemu ya Watumishi wa TMDA wakifurahia baada ya kupokea Tuzo, tarehe 29 Machi, 2025, Millenium Tower, DSM



Post a Comment

0 Comments