Vijana kama nguvu kazi ya
maendeleo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki wametakiwa kujifunza, kuipenda na kuisambaza
lugha ya Kiswahili ili kuifanya jumuiya hiyo kuwa imara na kudumisha umoja kwa
nchi zote.
Wito huo umetolewa na Mhadhiri mwandamizi na Mkuu wa Idara ya Taaluma za lugha kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Dkt. Onesmo Nyinondi wakiti akitoa wasilisho lake kwenye kongamano la kwanza la kimataifa la Kiswahili lililofanyika kwenye uwanja wa taifa wa sherehe za uhuru Kololo Kampala nchini Uganda.
“Vijana ukisikiliza wimbo wetu wa Jumuiya ya
afrika mashariki unazungumzia umoja wetu ndio nguzo yetu lakini ili tuweze
kufikia lengo hilo ni lazima tuwe na lugha moja inayotuunganisha wanajumuiya yote
ya afrika mashariki ili mtu anapotoka eneo moja kwenda kwingine kufanya
biashara au kutafuta maisha aweze kuelewana kwa lugha moja na sisi lugha yetu
ni Kiswahili” alifafanua Dkt. Nyinondi.
Aliongeza “ Umoja tunaouimba
unatoka wapi kama mtu akitoka Guru kwenda Mbarara haelewani lugha na watu wa
pale na akitoka Mbarara kwenda DRC kongo au Kenya hawezi kuwasiliana? Swala la
Kiswahili linahitaji msukumo wa kipekee ili kifahamike na kutumiwa na watu wote
ndani ya jumuiya yetu”.
Akitolea mfano maneno kwenye kitabu
cha mwanzo 11 msatari ule wasita kuhusu waliotaka kujenga mnara wa babeli na
baada ya Mungu kuona watu wale kwa umoja wao wanaweza kweli kufika mbinguni
aliwabadilishia lugha na hivyo kuwafanya washindwe kuelewana na hatimae ujenzi
wa mnara wa babeli ukakwama.
Dkt. Onesmo amesema umoja na maendeleo
ya Jumiya ya Afrika ya Mashariki yanawahitaji vijana ambao wanaongea lugha moja ya Kiswahili vizuri katika
shughuli mbalimbali ili kuondoa kikwazo cha lugha kwenye masuala ya
mashirikiano baina yao.
Aidha amependekeza kuwepo na
vitabu vidogovidogo ambavyo vinaeleza kwa Kiswahili mambo mbalimbali ya
makabila yaliyo ndani ya jumuia hiyo ili kila mmoja aweze kuelewa pamoja na
vitabu vyene istilahi zake kwenye shughuli mbalimbali za maendeleo.
Pia amependekeza kuwe na wiki ya
Kiswahili ili kuongeza uelewa kwa jamii kwenye jumuiya yote na kuona kuwa
pamoja na mipaka ya afrika mashariki lakini Kiswahili kiwe kiunganishi kikubwa
cha watu ndani ya jumuiya nzima.
Mhadhiri huyo kutoka SUA amesema mapinduzi
ya jambo lolote huanza na mtu mmoja na kisha kikundi na baadae jamii nzima
hivyo kila mmoja aanze kufikiria umuhimu wa lugha ya Kiswahili kwa maendeleo ya
watu maana penye nia pana njia.
Akitoa wasilisho lake
liliohudhuriwa na Balozi wa Tanzania nchini Uganda na Balozi wa Uganda nchini
Tanzania sambamba wawasilishaji wengine akiwemo Prof. PLO Lumbumba, Prof
A. Mtembei, Prof Wala na nguli wengine wa Kiswahili duniani na
kushirikisha watu wengine mbalimbali zaidi ya 8000 wakiwemo Wanasiasa, Maafisa
wa serikali, mabalozi, wasimamizi kutoka vyuoni, walimu, wanafunzi
Kongamano hilo lilihusisha washiriki kutoka nchi za Uganda, Tanzania, Kenya, Somalia, South Sudan, DRC, Rwanda, Burundi, Ghana, Nigeria and Canada.
0 Comments