About Me

header ads

Mahanaka Awataka Wananchi wa Mkuranga Kujitokeza kwa Wingi Kupiga Kura, Atoa Wito wa Kuwachagua Wagombea wa CCM

Mgombea Udiwani wa Kata ya Mkuranga kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Hamza Mahanaka, amewataka wananchi wa kata hiyo kuwachagua wagombea wote wa CCM ili kuendeleza kasi ya maendeleo katika maeneo yao.
Mahanaka ameyasema hayo leo wakati wa mkutano wa kufunga kampeni uliofanyika katika Viwanja vya Godauni, Mkuranga Mjini, ambapo amewashukuru wananchi kwa ushirikiano mkubwa waliouonyesha katika kipindi chote cha kampeni.

Aidha, Mahanaka amewahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi siku ya Jumatano, Oktoba 29, kutumia haki yao ya kikatiba ya kupiga kura, huku akiwatoa hofu kuwa vyombo vya dola vipo kwa ajili ya kulinda amani na usalama wa wananchi wote.

Amesema kuwa wananchi wanapaswa kujitokeza bila woga, kwani uchaguzi ni fursa muhimu ya kuamua mustakabali wa maendeleo ya eneo lao kwa kumchagua kiongozi sahihi kupitia CCM, chama ambacho kimeendelea kusimamia miradi ya maendeleo na ustawi wa wananchi.
“Tujitokeze kwa wingi, bila hofu wala mashaka. Vyombo vya ulinzi na usalama vipo kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa amani. Chagueni CCM kwa maendeleo endelevu ya Mkuranga,” alisema Mahanaka.








Post a Comment

0 Comments