Jeshi la Zimamoto na Uokoaji limewahakikishia Watanzania kuwa Matumizi ya Nishati safi ya kupikia ni Salama kwa Mazingira na Afya ya Binadamu Msemaji wa Jeshi hilo Naibu Kamishna Puyo Nzalayaimisi ameyasema hayo wakati wa mbio za pole pole zilizobeba Kampeni ya matumizi ya nishati hiyo ambayo ni "Matumizi ya Nishati safi ni salama" zilizofanyika Jijini Dodoma leo Februari 25, 2025
Mbio hizo zimehudhuriwa na Maafisa Wandamizi, Maafisa na Askari wa Jeshi hilo ambazo zilianzia Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na kuzunguka baadhi ya mitaa ya Dodoma na kumalizikia Makao Makuu ya Jeshi hilo.
Lengo la Kampeni hiyo ni kuwaasa Watanzania kutohofia juu ya matumizi ya nishati safi ya kupikia pamoja na kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe .Dkt. Samia Suluhu Hassan kuhusu matumizi ya nishati safi Aidha, Naibu Kamishna Nzalayaimisi amewataka wauzaji na wasambazaji wa nishati safi za kupikia kutoa elimu

0 Comments