Na Said Mwishehe,Michuzi TV
MKURUGENZI Mtendaji Mkuu wa Kampuni inayojihusisha na masuala ya Bima NewTan Insurance, Nelson Rwihula amesema wakulima wamekuwa wakikabiliwa na majanga mbalimbali na kujikuta wanapata hasara kubwa kutokana na kukosa Bima inayoweza kulipa fidia mazao yao.
Hivyo ameshauri wananchi ambao wanajihusisha na kilimo wameshauriwa kuweka utaratibu wa kukata bima itakatayowezsha kulinda mazao yao na kujikinga wakati wa majanga yanayoweza kuharibu mazao yao kwa
lengo la kuepuka hasara inayoweza kutokea.
Rwihula ameyasema hayo katika mkutano na waandishi wa habari, uliofayika leo Januari 21, 2025,Jijini Dar es Salaam, wakati akitangaza kuhusu kampuni hiyo yenye matawi tisa nchini, kuwa na jina jipya ambapo kwa sasa itaitwa NewTan Insurance badala ya jina la zamani la UAP Insurance, na kwamba mabadiliko hayo hayataathili utendaji wao wakazi kwani huduma zao zitaendelea kuboreshwa.
Rwihula ameeleza moja ya changamoto kubwa inayowakabili wakulima ni ukosefu wa elimu ya bima, nakwamba kampuni hiyo imejipanga kutoa elimu kwa wadau waliopo katika sekta hiyo.
Amefafanua kuwa kuna majanga mkulima anakuwa nayo kila siku, yakiwemo magonjwa, wadudu waharibifu, ukame na na mvua kubwa ambazo azizuiliki, yote hayo yanahitaji bima ili mkulima ajihakikishie usalama wake na mazao yake wakati wote.
Amesema kuwa katika kuhakikisha mkulima ananufika na kilimo wao wanaangalia ile hasara aliyoipata wanaenda kumpa fidia.
Wakati huo huo Frank Kajo ambaye ni Meneja wa Biashara za Benki wa Kampuni hiyo amtumia nafasi hiyo kueleza elimu ya bima inaweza kufika kwa urahisi zaidi kupitia vyama vyao vya ushirika na vikundi kwa kupitia matawi yao yaliyopo mikoani pamoja na mawakala wao.
Mwenyekiti wa Bodi Kampuni ya Newtan Insurance Bw. Moses Obonyo akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 20, 2025 jijini Dar es Salaam wakati wakitoa taarifa ya kubadilisha jina la kampuni kutoka jina la UAP Insurance Tanzania na kuwa Newtan Insurance
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Newtan Insurance Bw. Nelson Rwihula akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 20, 2025 jijini Dar es Salaam wakatoa taarifa ya kubadilisha jina la kampuni kutoka jina la UAP Insurance Tanzania na kuwa Newtan Insurance.
0 Comments