About Me

header ads

KAMATI YA BUNGE YAIPONGEZA CMA KWA UANZISHWAJI WA MFUMO WA KIDIJITALI.

 

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii imeipongeza  Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) kwa uanzishwaji wa Mfumo wa Uendeshaji na Usimamizi wa Mashauri kwa njia ya mtandao (Online Case Management System - OCMS) kwa wananchi.

Pongezi hizo zimetolewa leo Januari 21, 2025 na Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Fatma Toufiq wakati wa uwasilishwaji wa Taarifa ya utekelezaji wa Mfumo huo kwa Kamati hiyo jijini Dodoma.

Aidha, amesema wameona jitihada hizo za uanzishwaji wa mfumo huo ambao utarahisisha katika usikilizwaji wa mashauri kwa haraka na wakati na Utasaidia kuwafikia watu wengi.

Vile vile amepongeza jitihada za serikali ya awamu ya sita ya Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kwa utendaji kazi kwa ajili ya ustawi na maendeleo ya wananchi wa Tanzania yanavyopatikana kwa ufanisi mkubwa.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) Mhe. Usekelege Mpulla amesema mfumo upo mbioni kuzinduliwa na utaweza kuwaruhusu wafanyakazi na waajiri kufungua mashauri wakiwa mahali popote bila kulazimika Kwenda katika ofisi za Tume.



 

Post a Comment

0 Comments