Na Jane Edward,Arusha
Akizungumza na waandishi wa habari Mariam Kobelo Meneja wa Idara ya Utalii na Masoko NCAA amesema mamlaka ya Ngorongoro imeamua kuanzisha kampeni hiyo kwa mwaka huu kuweza kuongeza idadi ya watalii wa ndani na kuwezesha watanzania kuwa sehemu ya kufahamu vivutio vilivyopo katika hifadhi hiyo.
Amesema kuwa idadi ya watalii wa ndani wanaotembelea eneo la hifadhi hiyo ni ndogo kulinganisha na wageni wanaokuja kutoka Mataifa mbalimbali duniani hali iliyopelekea kuona umuhimu wa kuwezesha watanzania kutembelea maeneo hayo yanayosimamiwa na hifadhi hiyo.
"Takwimu hii inaonyesha wazi kuwa mwamko wa watanzania kutembelea maeneo ya hifadhi bado ndogo na hivyo kuhitajika msukumo wa sisi kama mamlaka kufanya jitihada za makusudi za uhamasishaji wa wananchi"Alisema
Akizitaja fursa za watanzania watakazozipata wakati wakiwa katika eneo la hifadhi hiyo ni pamoja na kutembelea kreta ya Ngorongoro,Kreta ya Empakai na Olmoti,Msitu wa nyanda za juu kaskazini ambao ni makazi ya wanyama wengi ikiwemo ikiwemo Simba,Tembo,Faru,Nyati na Chui.
0 Comments