About Me

header ads

 

DAR ES SALAAM

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe, Dkt. Selemani Jafo ametoa maelekezo kwa katibu Mkuu wizara hiyo kushughulikia changamoto zote zinazowakabili wafanyabiashara ili kusaidia uwekezaji uende kwa haraka, na kuyataka makampui kuzalisha bidhaa zinazokidhi mahitaji na kujihepusha kufanya udanganyifu

Amesema Serikali ya Awamu ya sita inaendelea kuboresha miundombinu ili sekta ya Biashara iwe na ushindani wenye viwango vya Kitaifa na Kimataifa.

Waziri Jafo ameyasema hayo katika Maadhimisho ya kitaifa ya siku ya ushindani Duani yaliyofanyika leo Disemba 5, 2024 Jijini Dar es Salaam.

Aidha, Dkt. Jafo ameagiza mijadala yote itakayojadiliwa katika maadhimisho hayo iwasilishwe kwake ndani ya siku kumi na nne ili kufanyia kazi mawazo yaliyojadiliwa, kwa lengo la kuongeza kasi katika kushughulikia changamoto zote zitakazo ibuliwa kwenye mijadala hiyo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Tume ya FCC Dkt Aggrey Mlimuka amesema kuwa Tume hiyo inawajibu wa kusimamia uwepo wa fursa sawa kwa washindani wakubwa na wadogo katika soko, na kupunguza ukiritimba katika masoko kwa kuhakikisha washindani wakubwa hawazuii washindani wadogo kukua na kuingia au kuwatoa sokoni.

Nae Mkurugenzi Mkuu wa FCC, Wiliam Erio amesema maadhimisho hayo ya siku ya ushindani Duniani ni ya kwanza  tangu kufanyika kwa marekebisho ya sheria nchini.

"Tunamshukuru sana Rais samia Suluhu Hassan na Spika wa Bunge kwa kufanikisha kupitishwa kwa marekebisho na kuwa sheria jambo ambalo litatuwezesha kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.

kila ifikapo Disemba 5 kila mwaka, Dunia huadhimisha siku ya ushindani Duniani ambapo kwa Tanzania maadhimisho hayo yamefanyika Jijini Dar es salaam yakiwa na Kaulimbiu isemayo "Sera ya Ushindani na kudhibiti kukosekana kwa usawa katika uchumi"

Post a Comment

0 Comments