About Me

header ads

Mashujaa wa Kansa ya Matiti watoa umuhimu wa kuanza matibabu ya kansa mapema

 

 

Yataka watu kuacha tiba za waganga kienyeji katika kuokoa maisha yao.

Na Chalila Kibuda ,Michuzi TV

  
Mashujaa wa Kansa ya Matiti wameitaka wamewataka wanawake kupima mara kwa mara na wanapogundulika kuanza matibabu katika dalili awali ambazo kupona ni asilimia 100.

Wakizungumza katika katika Mafunzo ya Wanafunzi Madaktari katika  Taasisi ya Saratani Ocean Road  jijini Dar es Salaam wamesema wenyewe kupona kulitokana na kuwahi kutokana na kuwahi kwao na kufuata taratibu za matibabu.

 Shujaa wa Saratani ya Matiti Habiba Hassan amesema kuwa mama yake alifariki kwa saratani ya matiti ndio ilikuwa somo kutokana yeye alipoona dalili kama zile za mama yake alikimbia haraka Hospitali kuna kugundulika akiwa na mimba na baada ya kujifungua alifanya oparesheni ya kukatwa titi moja na kuanza matibabu mpaka amepona na kuendelea na maisha yake kama kawaida.
Amesema kuwa baadhi ya wanawake wakiona dalili hizo hukimbilia kwa waganga wa jadi ambao wanatumia muda mwingi kutumia dawa ambazo haponi na kwenda hospitali katika dalili za katika hatua ya nne ambapo hupoteza maisha.

Amesema kuwa saratani inatibika kinachotakiwa mara baada ya kugundulika kuanza matatibabu ambayo kupata kwa kipindi kifupi na kupona kuendelea na maisha.

Jasmin Said amesema kuwa yeye alipona dalili za mchubuko katika ziwa alikwenda Hospitali na kupewa dawa na baada ya hapo hali ilikuwa mbaya hali ambayo ilifanya familia kutafuta dawa za jadi hali ikawa mbaya zaidi na baada ya hapo akalazimika kupima na kundulika na kansa ambapo alianza matibabu akiiwa amechoka kutokana na kutumia dawa nyingi ambazo hazikuwa sahihi kutibu.

Amesema  alipofika Ocean Road alianza matibabu na baadae kukatwaa ziwa lakini anashukuru kupona na kuendelea na maisha na kushauri wanawake kupima mara kwa mara na watapobainika kuanza matibabu katika hatua ambayo kupona ni asilimia 100.

Amesema kuwa alikuwa mtoto mmoja lakini baada ya kupona daktari akaomba ushauri juu kuzaa mtoto mwingine akaambiwa anaweza kuendelea kuzaa watoto.

Mratibu wa Masuala ya Afya ya Jamii wa Chama cha Wanafunzi  Madaktari Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (TAMSA-MUHAS) Avith Kibani amesema kuwa ni utaratibu wa kutembelea vyuo na wanafunzi wa Sekondari katika kutoa elimu ya masuala ya afya kwa kuamini kuwa watakuwa na misingi ya kujua afya zao katika ujenzi wa Taifa kwani Taifa linahitaji vijana wenye afya katika ujenzi wake.

Mwenyekiti wa Chama cha Madaktari Wanawake Tawi la Chuo kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi (MEWATA-MUHAS) Atupele Kuponda amesema kuwa kwenda Taasisi ya Ocean Road kujifunza masuala mbalimbali na kupata picha ambapo baada ya kuhitimu watajua namna ya kusaidia wagonjwa wa saratani.

Amesema kuwa unataratibu wa kutembelea maeneno mbalimbali kama wanafunzi wanakuwa wanajua jamii ilivyo katika afya kwani vijana watakuwa sehemu ya maamuzi wakiwa miongozo ya kuwaongoza.

Wakati akifungua mafunzo ya Wanafunzi Madaktari kutoka Vyuo Mbalimbali Daktari na Mtaalam wa Afya ya Jamii wa Taasisi ya Ocean Road Dkt.Chacha Josiah amesema kuwa  mafunzo kwa wananfunzi ni muhimu kutokana na baadae kuwa sehemu ya maamuzi ya kufanya kazi zao katika misingi thabiti.

Mratibu wa Masuala ya Afya Afya ya Jamii wa Chama cha Madatari wa Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shurikishi Muhimbili (TAMSA-MUHAS) Avith Kibani akizungumza kuhusiana na mafunzo kutoka Taasisi ya Oceon Road jijini Dar es Salaam.
Daktari na Mtaalam wa Afya ya Jamii wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road Dkt.Chacha Josiah  akizungumza wakati akifungua mafunzo kwa wanafunzi wa Udaktari waliotembelea Taasisi  hiyo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Chama cha Wanafunzi Madaktari Wanawake  wa Tawi la Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MEWATA-MUHAS) Atupele Kuponda akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na umuhimu wanafunzi madaktari kutembelea Taasisi ya Saratani ya  Ocean  Road ,jijini Dar es Salaam.
Daktari wa Saratani wa Taasisi ya Saratani  Ocean Road Dkt.Ludovic Fred akizungumza  kuhusiana na wanafunzi wa Udaktari kutembelea Taasisi ya Saratani Oceon Road jijini Dar es Salaam.
Shujaa wa Kansa ya Matiti Habiba Hassan akizungumza  na waandishi wa habari katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road  kuhusiana kuchukua hatua za haraka katika kutibu kansa hadi kupona ,jijini.Dar es Salaam.
Shujaa wa Kansa ya Matiti Jasmin Said akizungumza  na waandishi wa habari katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road  kuhusiana kuchukua hatua za haraka katika kutibu kansa hadi kupona ,jijini.Dar es Salaam.

Post a Comment

0 Comments