About Me

header ads

MADEREVA WATAKIWA KUZINGATIA TIJA, UFANISI KATIKA UTENDAJI KAZI WAO

 

Na. Mwandishi wetu - Dar es salaam.


Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Zuhura Yunus, amewataka Madereva kuzingatia tija na ufanisi katika utendaji kazi wao ili kuhakikisha jamii inafanya kazi  za kiuchumi kwa usalama na muda muafaka, hivyo kukuza uchumi  wa mtu mmoja na Taifa kwa ujumla.

Amebainisha hayo wakati wa  kufungua Mafunzo ya Tija na Ufanisi wa Madereva, leo Oktoba 29,  2024 Jijini Dar es salaam.

"Nchi yetu inakabiliwa na changamoto za ajali barabarani ambazo zinaathiri nguvu kazi ya Taifa na kupunguza pato, hivyo basi ni muhimu kuzingatia mafunzo haya ili kupunguza ajali ambazo zinaweza kuepukika" amesema.

Akizungumza Mkurugenzi wa Ukuzaji Tija, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Yohana Madadi, amesema lengo la Mafunzo hayo ni kutoa ujuzi na mbinu za udereva bora ili kupunguza ajali barabarani na kutii sheria bila shuruti.

Kwa upande wake Meneja Uratibu na Mazingira  Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) Geofrey Silanda, ameipongeza Ofisi ya Waziri ya Mkuu kwa kuandaa mafunzo hayo, ambayo yakikamilika yataongeza ufanisi na tija  katika utendaji kazi wao.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Zuhura Yunus, akifungua Mafunzo ya Ustadi wa Kuboresha Tija na Ufanisi kwa Madereva, leo Oktoba 29, 2024 Jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa Ukuzaji Tija Ofisi ya Waziri Mkuu -Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Yohana Madadi akizungumza wakati wa Mafunzo ya Ustadi wa Kuboresha Tija na Ufanisi kwa Madereva, leo Oktoba 29, 2024 Jijini Dar es salaam.
Wakurugenzi Ofisi ya Waziri Mkuu -Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu wakifuatilia Mafunzo ya Ustadi wa Kuboresha Tija na Ufanisi kwa Madereva, leo Oktoba 29, 2024 Jijini Dar es salaam.

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Zuhura Yunus, akiwa katika picha ya pamoja na Wakurugenzi Ofisi hiyo, pamoja na Madereva walio hudhuria Mafunzo ya Ustadi wa Kuboresha Tija na Ufanisi kwa Madereva, leo Oktoba 29, 2024 Jijini Dar es salaam.



 

Post a Comment

0 Comments