Tanzania, 10 Septemba 2024. Mradi wa Ubunifu wa FUNGUO unaotekelezwa na UNDP hapa Tanzania kwa ufadhili wa na Umoja wa Ulaya na mfuko waIMBEJU wa CRDB Bank Foundation, imeamua kushirikiana ili kubadilisha mwenendo wa ufadhili wa wajasiriamali wabunifuhapa nchini.
Ushirikiano huu wa kimkakati unalenga kutumiaruzuku inayotolewa na Umoja wa Ulaya kwa kampuni changa nakufungua fursa ya kupata mikopo ya riba na masharti nafuukutoka kwa CRDB Bank Foundation, ili kuongeza uwezo wakimtaji kuwawezesha wajasiriamali kukua kwa haraka zaidi.
Tangu kuanziswa kwake mwaka 2022 kwa ufadhili kutoka Umoja wa Ulaya kupitia mpango wa BEGIN unaoratibiwa na kitengacha mazingira ya biashara katika Ofisi ya Rais – Mipango naUwezeshaji, FUNGUO imewekeza zaidi ya TZS bilioni 3.8 katika kampuni changa 43, ikichangia katika kutengeneza nakuendeleza takribani ajira 4000 za moja kwa moja na zisizo za moja kwa kwa vijana wa Tanzania.
Dhamira ya mpango huu nikuongeza idadi ya kampuni za ubunifu zenye uwezo wa kustawiharaka ili kuharakisha kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevuya Tanzania. Wafadhili wengine wa mradi wa FUNGUO nipamoja na Serikali ya Uingereza kupitia mpango wa Africa Technology and Innovation Partnerships (ATIP) na UNDP katikamkakati wake wa kuwawezesha vijana kiuchumi.
Mwaka huu, FUNGUO imepanga kutoa hadi TZS bilioni 1.4, ikilenga kwa makusudi kuwawezesha wanawake walioanzishabiashara zenye ubunifu ndani yake. Angalau asilimia 40 yaufadhili uliopo umetengwa kwa ajili ya biashara zinazomilikiwa na kuongozwa na wanawake, ikiwa ni ongezeko la asilimia 30 ukilinganisha na mwaka jana, ili kutilia mkazodhamira ya ujumuishi wa kijinsia na kuunga mkono uongozi wawanawake katika ubunifu.
Ufadhili huu unalenga biashara changa bunifu zinazoongozwa na vijana ambazo zinamilikiwa kwa wingina raia wa Tanzania.
FUNGUO na IMBEJU hazitoi tu msaada wa kifedha, bali pia zinawawezesha wajasiriamali vijana, wanawake, na makundimaalum kwa kuwapa zana muhimu za kubadilisha mawazo yaoya biashara kuwa miradi yenye mafanikio na yenye athari kubwakwa jamii.
Ufadhili wa mwaka huu kutoka FUNGUO naIMBEJU utawekeza katika kujenga mchakato unaovutia mifumomingine ya kifedha nchini, ikiwemo wawekezaji binafsi na taasisinyingine za kifedha.
Katika hotuba yake kama Mgeni Rasmi, Mheshimiwa Stanslaus Haroon Nyongo (MB), Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Mipango na Uwekezaji, alieleza kuwa "Vijana wa Tanzania nirasilimali kubwa kwa taifa, wamejaa mawazo ya kibunifu namaarifa ya kutengeneza mustakabali ulio bora zaidi kwa taifaletu.
Kwa kuwawezesha na mitaji ya kuanzisha na kuendelezabiashara zao, msaada wa kitaalamu, mafunzo, na kadhalika, vijana wetu wanakuwa wamepata zana wanazohitaji kujengabiashara zenye mafanikio na zinazoweza kukua kwa haraka nakuchangia uchumi.
Hili ni muhimu tunapolenga kukuza sektabinafsi yenye nguvu inayoweza kutengeneza ajira nakuhamasisha ibunifu katika uchumi wetu. Ningependakuwashukuru washirika wetu wa maendeleo, Umoja wa Ulaya, Serikali ya Uingereza na UNDP kwa kuunga mkono miradi yaaina hii."
Bi. Christine Grau, Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania, amesisitiza dhamira ya Umoja wa Ulaya katika kukuza mazingiraya biashara yanayochochea ukuaji wa ubunifu nchini Tanzania. "Ni dhahiri ya kuwa Mpango wa FUNGUO ni ushahidi wakujitolea kwetu kusaidia wajasiriamali wa Kitanzania kufikiamafanikio.
Tunaamini ushirikiano huu na IMBEJU utaimarishamfumo wa ujasiriamali nchini Tanzania, ukileta manufaa halisikwa wajasiriamali na uchumi kwa ujumla," alisema.
Kwa upande wake Bw. Muyeye Chambwera, Naibu Mwakilishi Mkazi wa UNDP Tanzania, alionyesha dhamira yaUNDP ya kuwawezesha vijana kupitia mipango mbalimbali.
Bw. Chambwera alisema kuwa "UNDP imejitolea kusaidia vijanakutambua uwezo wao, na kufungua milango ya upatikanaji wafedha kupitia miradi yao. Tunaamini tunaweza kuleta atharikubwa kupitia ushirikiano huu na CRDB Bank Foundation ambaoni ushahidi wa juhudi nyingi tunazofanya kufungua milango zaidiya kufanya kazi pamoja na wadau mbalimbali."
Naye Bi Tully Esther Mwambapa, Mkurugenzi Mtendaji waCRDB Bank Foundation, alisisitiza uwezo wa mabadiliko waushirikiano huu kwa biashara za vijana.
"Mpango wa IMBEJU umejizatiti kwa dhati kuwawezesha kizazi kijacho cha wajasiriamali wa Kitanzania. Kwa kuunganisha ujenzi wa uwezo, elimu ya kifedha, na maendeleo ya ujuzi wa ujasiriamali, IMBEJU haipatii msaada wa kifedha tu, bali tunatoa mfumokamili utakaokuza vipaji vya vijana.
Ushirikiano huu na FUNGUO unaongeza juhudi zetu za kuboreasha mazingirayanayosaidia biashara zinazomilikiwa na vijana kufanikiwa.
Tunaamini kuwa kwa kuwapa wajasiriamali vijana zanawanazohitaji, tunajenga msingi wa mazingira thabiti na endelevuya ujasiriamali nchini Tanzania," alisema Bi. Mwambapa.
Wakati wa kutambulisha Mpango wa FUNGUO, Joseph Manirakiza, Meneja wa Mpango, alisisitiza njia jumuishi yakusaidia wajasiriamali. "FUNGUO haitoi ruzuku za mitaji, balitumewekeza pia kwenye mfumo mpana wa kustawishaujasiriamali na ubunifu, unaojumuisha usaidizi wa kiufundi, ushauri, na fursa za kujenga mitandao.
Lengo letu nikuwawezesha wajasiriamali wa Kitanzania kukabiliana nachangamoto huku tukitumia njia zote zinazowezekana ili biasharazao ziweze kufikia ukuaji endelevu. Ushirikiano wa kimkakatikama huu na CRDB Foundation unatufanya twende hatua mojambele zaidi ya kufungua uwezo kamili wa biashara za ubunifu nchini Tanzania," alielezea.
Bw. Richard Craig, Mkuu wa Idara ya Uchumi katika Ubalozi waUingereza, alisisitiza dhamira ya Uingereza ya kuendelea kushirikiana na Tanzania kwa ajili ya kuhakikisha Uchumi wanchi unakua. Akizungumza katika uzinduzi huo, alisema: "Programu ya FUNGUO ni sehemu ya ushirikiano mpana wakiuchumi kati ya Uingereza na Serikali ya Tanzania, kamailivyoainishwa katika Ushirikiano wetu katika Ufanisi waPamoja. Biashara changa bunifu ni muhimu katika njia ya ukuajiwa uchumi shirikishi.
Tunaposaidia biashara hizi, tunaongezauwezo wa kutengeneza ajira na kuchochea suluhisho zilizo za kibunifu katika kukabiliana na changamoto zinazotucheleweshakufikia maendeleo maendeleo."
Dirisha la maombi ya ufadhili huu litafunguliwa rasmi kuanziatarehe 10 Septemba 2024 hadi tarehe 09 Oktoba 2024. Biasharazenye ubunifu (startups) na SMEs zinazostahiki zinahimizwakuomba na kutumia fursa hii kupata ufadhili na msaada wakukuza biashara zao zinazochochea mabadiliko katika jamii.
0 Comments