Na Chalila Kibuda,Michuzi.
Jukwaa la usimamizi wa mtandao Tanzania Internet Governance Forum(TzIGF) limesema kuwa kuna umuhimu wa kuangalia sera ya nchi katika masuala ya mitandao kutokana na Mapinduzi ya Teknolojia zinaweza kuwa zimepitwa na wakati.
Wakizungumza katika Jukwaa lililoandaliwa na Taasisi ya internet Society Tanzania Chapter(ISOC-TZ) lililokutanisha vijana na wadau mbalimbali walisema Teknolojia inakwenda kwa hivyo kuna ulazima wa kutazama sera za nchi kama zinakidhi kukimbinzana na Mapinduzi ya teknolojia hiyo.
Danford Mbarama kutoka Kitengo cha Miundombinu wa Wizara ya Habari , Mawasiliano na Teknolojia ya Habari amesema katika kuendana na ukuaji wa Teknolojia ya Mawasiliano Serikali imewekeza katika Ujenzi wa miundombinu ya mkongo wa Taifa ambao umefika katika kila Wilaya.
Amesema kuwa katika usimamizi wa mtandao salama kwa watumiaji watumie katika kujijenga kimaendeleo.
Mtaalam wa Blockchain and cryptocurrency Miriam Shaka amesema kuwa usimamizi wa mitandao na ukuaji wa Teknolojia lazima vijana kujijengea uwezo ili kutumia katika mazingira salama.
Amesema kuwa mabadiliko sera ya mtandao ambayo itakwenda na Mapinduzi ya Teknolojia ya kufanya hakuna mtu kuanchwa nyuma.
Diwani wa Viti Maalum Mkoa wa Dar es Salaam Elizabeth Edward amesema kuwa mitandao imeweza kuweka wazi vitu vingi ambavyo taarifa zake zilikuwa haziwekwi wazi.
Amesema katika usimamizi huo kama watunga sera wanakwenda kuangalia sera na kama haziendani na mazingira ya sasa kuweza kushawishi zibadilishwe.
Amesema kuwa vijana mitandao watumie katengeneza fursa za ajira na sio kuingilia faragha za watu na kushirikisha watu wengine.
Rais wa ISOC -Tz Nazar Kirama amesema vijana ndio viongozi wa sasa hivyo wanahitaji kujengewa uwezo katika masuala ya usimamizi wa mitandao.
Amesema vijana wana nguvu ya kushawishi serikali kuweka usawa wa matumizi ya internet vijijini na mjini pamoja na kushauri gharama za vifurushi kushuka ili kila mtanzania aweze kupapta huduma za mawasiliano.
"Vijana wakijengewa uwezo katika usimamizi wa mtandao pamoja na kusimamia mtandao ndio daraja la kufanya kuwepo usawa wa matumizi kutokana vijana kuwepo katika sehemu za maamuzi na kufanya kurahisisha michakato yake"amesema Kirama
Hata hivyo amesema kuwa katika upatikanaji wa huduma za mtandao katika baadhi ya maeneo hawapati kwa ubora ambapo jukumu la vijana hao wanawajibu kushauri watunga sera juu ya kupata uwiano.Mhandisi Danford Mbarama wa Kitengo cha Miundombinu wa Wizara ya Habari , Mawasiliano na Teknolojia ya Habari akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na Jukwaa la Usimamizi wa Mtandao ulioandaliwa na Taasisi ya Internet Society Tanzania Chapter (ISOC) uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Rais wa Internet Society Tanzania Chapter (ISOC)Nazar Kirama akizungumza na Waandishi umuhimu wa Jukwaa la Usimamizi wa Mtandao,Jijini Dar es Salaam.
Miriam Shaka wa Block chain and cryptocurrency akizungumza kuhusiana usimamizi wa mitandao na kuangalia sera za nchi ,jijini Dar es Salaam.
0 Comments