About Me

header ads

ORYX YAGAWA MITUNGI YA GESI 700 KWA WANANCHI MKOANI RUVUMA

Na Mwandishi Wetu,Ruvuma


KAMPUNI ya Oryx Gas Tanzania kwa kushirikiana na Naibu Waziri wa Nishati Judith Kapinga wamegawa mitungi ya gesi ya Oryx 700 yakiwa na majiko yake kwa wananchi wa Mbinga na Namtumbo mkoani Ruvuma.

Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi mitungi hiyo Naibu Waziri Kapinga ambaye ni Mbunge wa Viti Maalum amesema Serikali kupitia Wakala wa Nishati Bijijini(REA)kwa mwaka wa fedha 2024/2025,imepanga kutumia Sh.bilioni 10  kununua majiko banifu(Gesi) takribani  400,000 ambayo yatasambazwa kwa wananchi.

Pia amesema lengo la Serikali ni kuongeza matumizi ya Nishati safi ya kupikia nchini kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ya utunzaji wa mazingira na mabadiliko ya tabia ya nchi na kuepusha wananchi kupatwa na maradhi yanayotokana na matumizi ya nishati ya kuni na mkaa.

"Hadi sasa Serikali kupitia Wiizara ya Nishati imeshatoa  majiko 83 yenye thamani ya Sh.bilioni 3.5 na kazi ya kugawa majiko hayo inaendelea lengo likiwa ni kupunguza gharama za vifaa vya nishati safi ya kupikia ili wananchi wapate huduma hiyo kwa  gharama nafuu."

Akizungumza mchango wa Oryx katika kuhamasisha matumizi ya nishati safi ameipongeza Kampuni kwa namna ambavyo imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha wananchi wanatumia nishati safi hasa majiko ya gesi na kuachana na kutumia nishati chafu ya Kuni na mkaa.

Awali  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Oryx Gas  Tanzania Ltd Benoit Araman amesema lengo la kampuni hiyo ni kuunga mkono juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan za kufanikisha wananchi wanatumia nishati safi ya kupikia.

Aidha amesema kuwa Watanzania 33,000 wanapoteza maisha kila mwaka kwa kuvuta moshi na chembechembe zitakonazo na mkaa na kuni,lakini kwa kutumia Gesi ya Kampuni ya Oryx Gesi wataweza kuepukana na tatizo hilo.

Araman amesema uulinzi wa mazingira kupika kwa kutumia gesi ya Oryx kutazuia ukataji  ovyo wa miti,kwa hiyo itasaidia kulinza mazingira na ukitumia gesi utapika kwa haraka na kwa ufanisi na wanawake watakuwa na muda wa kufanya kazi za kujiletea maendeleo.

Kwa upande wake Meneja miradi nishati safi ya kupikia wa kampuni ya Oryx Peter Ndomba amesema kampuni hiyo imeweka mipango yakinifu kuhusu  namna ya utunzaji wa mazingira sambamba na kutoa elimu kwa wananchi ambayo ni endelevu ili kila mwananchi aweze kupata uelewa juu ya  umuhimu wa nishati safi ya kupikia.

Ndomba amesema hayo jana wakati akikabidhi majiko 300 ya kupikia kwa Mbunge wa Jimbo la Namtumbo Vita Kawawa kwenye ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Dkt Samia Suluhu Hassan.

Amesema tayari kwa mkoa wa Ruvuma jumla ya majiko banifu 1,000 yametolewa kati ya majiko hayo 700 yamegawiwa wilaya ya Mbinga na 300 wilaya ya Namtumbo lengo ni kusaidia kutoa elimu kwa wananchi juu ya matumizi bora ya nishati safi na kwamba zoezi hilo litaendelea katika mikoa mingine hapa nchini.

Wakati huo huo Mbunge wa Jimbo la Namtumbo mkoani Ruvuma Vita Kawawa,amewataka wananchi kuona umuhimu wa kutumia nishati safi na kuacha kutumia nishati ambazo siyo rafiki kwa mazingira.







 

Post a Comment

0 Comments