Na Nasra Ismail, Geita
Wananchi katika mikoa ya kanda ya ziwa yaani Geita,Kagera,Mara, Sinyanga na Simiyu pamoja na mikoa jirani watarajiwa kunufaika na mpango wa kuanzishwa kwa kituo mahiri cha utoaji wa huduma za kibingwa na ubingwa bobezi za magonjwa ya moyo katika hospitali ya kanda ya Chato ambapo hapo awali huduma hizi walizipata kwa kusafiri umbali mrefu kupata huduma hizi.
Huduma hizi ambazo zinatarajiwa kuanza julai 15 mpaka julai 17 zitahusisha uchunguzi wa matibabu ya magonjwa ya presha, sukari magonjwa ya moyo, pamoja na mishipa ya damu ambapo pia wananchi watanufaika kwa kupata elimu ya lishe bora kutoka kwa wataalamu ambayo itawasaidia kupunguza magonjwa haya yasiyoambukiza.
Kwa upande mwingine serikali inatarajia kuanzisha ujenzi wa jengo la upasuaji wa moyo na mishipa ya damu katika hospital ya Rufaa ya kanda ya Chato ambapo huduma zote za upasuaji zinazotolewa katika taasisi ya Jakaya Kikwete zitaanza kutolewa hospitalini hapo.
Aidha uwepo wa kituo hiki utasaidia kupunguza vifo dhidi ya magonjwa yasiyoambukiza pamoja na kupunguzia ghalama ambazo mwanzo walizitumia kufata matibabu haya jijini Dar es salaam.
Afisa habari katoka Hospital ya Kanda Chato Husna Kamangi amesema kua hospitali iliingia makubaliano na taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete(JKCI) chini ya wizara ya afya ili kushirikiana katika kuanzisha,kuendeleza pamoja na kuimarisha huduma za matibabu ya magonjwa ya moyo kwa wananchi wa kanda ya ziwa.
”huduma za uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya moyo zilianzishwa rasmi novemba 2022 kattika hospitali ya rufaa ya kanda ya chato ambapo katika kipindi cha mwaka 2022-2023 zaidi ya wanancchi 2000 walipimwa afya ya moyo na mwaka 2023-2024 idadi ya wananchi waliojitokeza kupata huduma hii imeongezeka na zaidi ya wananchi 3400 wamepimwa na kati yao wananchi 576 waligundulika kuwa na matatizo ya presha, sukari, na magonjwa ya moyo ambao walipatiwa matibabu na wengine kuendelelea kuwa chini ya madaktari bingwa bobezi kutoka taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete wanaifika kila juma la tatu la mwezi katika hospital ya rufaa ya kanda ya Chato kutoa huduma hizi ” Kamangi
0 Comments