About Me

header ads

SERIKALI KUSIMAMIA MISINGI YA SHERIA, SERA KUIMARISHA HUDUMA ZA FEDHA KWA GHARAMA NAFUU,KUPANUA WIGO

Na Mwandishi Wetu

WIZARA ya Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari imesema Serikali itaendelea kusimamia misingi ya Sheria, Sera na Kanuni za usimamizi wa sekta ya fedha ikiwemo kuongeza upatikanaji wa huduma za kifedha kwa gharama nafuu kwa kupanua wigo wa matumizi ya TEHAMA katika utoaji wa huduma za kifedha.

Hivyo  kuongeza huduma jumuishi za fedha nchini hususan wa kipato cha chini na waishio vijijini ambako huduma za kifedha hazipatikani kwa urahisi.

Akizungumza katika utiaji saini mkataba wa kibiashara kati ya Shirika la Posta Tanzania na Azam Pesa,Naibu wa  Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Maryprisca Mahundi amesema Serikali itaendelea kuboresha na kupanua matumizi ya TEHAMA katika huduma za kifedha.

"Serikali itaendelea kuboresha mifumo ili kuhakikisha huduma zinazowezeshwa na TEHAMA kama huduma za kifedha zinajumuisha wananchi wote na haya ni matokeo ya ukuaji wa TEHAMA na miundo ya kitaasisi ambayo ni wezeshi."

Kwa upande wake Maharage Ally Chande ambaye ni  Postamasta Mkuu amesema mahusiano haya na huduma hiyo itasaidia kuhudumia wateja lakini pia kuongeza mapato ya shirika, sambamba na kuimarisha mzunguko wa kifedha kwa wananchi.

Awali  Ibrahim Malandi ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Azam Pesa na Mwakilishi wa kampuni za Said Salim Bakhresa amesema Serikali imekua ikisaidia na kuunga mkono juhudi za huduma mbalimbali za kifedha hasa za kidigital na zinazoendana na teknolojia na mahitaji ya dunia jambo linalotoa fursa kwa wawekezaji kundelea kuwekeza zaidi.

Kwa kukumbusha tu Azam pesa inatoa huduma za kifedha za kutoa na kuweka pesa kwa kutumia pochi kidigital kupitia simu janja na inatoa huduma bora na nafuu na ushirikiano huo na shirika la posta Tanzania  ni nafasi muhimu ya kuhakikisha huduma hizi zinakua kwa kasi na hivyo kufikia ujumuishaji wa kifedha.
Postamasta Mkuu Maharage Ally Chande akizungumza wakati wa utiaji saini mkataba wa kibiashara kati ya Shirika la Posta Tanzania na Azam Pesa leo Jiji Dar es Salaam.
     Kutoka kulia; Postamasta Mkuu,Maharage Ally Chande  Mkurugenzi Mtendaji wa azampesa,Ibrahim Malando pamoja na mapema leo wakitia saini mkataba wa ushirikiano wa kibiashara baina ya Shirika la Posta Tanzania na Azam Pesa.

Post a Comment

0 Comments