Adhabu hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Rahim Mushi wa Mahakama Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, baada ya mshtakiwa kusomewa shitaka na kukiri kutenda kosa hilo.
Hakimu Mushi amesema kabla ya kutoa hukumu hiyo, amezingatia shufaa za pande zote mbili ikiwemo kwamba mshtakiwa ni mkosaji wa mara ya kwanza .
"Mshtakiwa huyu hakuisumbua mahakama kwani alikiri shtaka pamoja na hoja za awali alizosomewa hivyo ameokoa muda wa mahakama kusikiliza kesi hii kama angekana shtaka,"amesema Hakimu Mushi
Amesema, mshtakiwa baada ya kukiri kosa lake mahakama inamtia hatiani katika kosa la kufanya biashara bila kibali cha BoT, kwa hiyo atatakiwa kulipa faini ya sh milioni mbili na akishindwa atatumikia kifungo cha miaka mitano.
Hata hivyo, mshitakiwa huyo alifanikiwa kulipa faini na kuachiwa huru na Mahakama.
Pia, mahakama hiyo imetaifisha sh 16,797,000 na Dola za Marekani 64,255, Yuen 500 alizokamatwa nazo kuwa mali ya Serikali ya Tanzania.
Awali, akimsomea shitaka lake,Wakili wa Serikali Mwandamizi Christine Joas alidai, mshtakiwa alitenda kosa hilo kati ya Januari hadi Mei 16 mwaka huu katika duka kubwa (Supermarket) , iitwayo Peninsula iliyopo eneo Oysterbay, Kinondoni Dar es Salaam.
Imedaiwa kuwa, mshtakiwa akiwa eneo hilo alikutwa akifanya biashara ya kubadilosha fedha za kigeni bila kuwa na leseni kuyoka BoT.
Pia, Imedaiwa kuwa, Mei 16, mwaka huu mlalamikaji aliweka mtego na kumpa msiri fedha za Tanzania aende kuzibadilisha kwa mshtakiwa ambazo zilikuwa noti za sh.10,000 281 sawa na sh milioni 2.81.
Amedai kuwa msiri alikwenda na bila wasiwasi mshtakiwa alibadili fedha hizo, msiri alitoa taarifa polisi, ambapo walifika na kumkamata mshtakiwa.
"Baada ya kukamatwa upekuzi ulifanyika ,alikutwa na fedha hizo za mtego, noti mbalimbali za kigeni kiwemo noti 627 za Dola za Marekani 100, noti 22 za dola 50, noti 7 za dola 5, noti 18 za dola 10, noti 102 za sh 10,000 na fedha za China Yuen 500,"amedai
Imedaiwa kuwa , noti 281 za sh 10,000 alizokamatwa nazo mshtakiwa zilifanana na fedha za mtego na baada ya upekuzi fomu ya kukamata mali ilijazwa, mshtakiwa na polisi waliokuwa katika upekuzi waliisaini.
Mshitakiwa huyo alifikishwa mahakamani na kufunguliwa kesi hiyo.
0 Comments