Na Ashrack Miraji Lushoto Tanga
MKUU wa Wilaya ya Lushoto mkoani Tanga Jafar Kubecha amewaomba radhi wananchi na wageni wote waliotarajia kudhuhuria katika tamasha la kitalii la "Usambara Tourism Festival" lenye lengo la kukuza uchumi hasa kwenye sekta ya utalii wilayani hapo.
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Mkuu wa Wilaya Kubecha amesema tamasha hilo lililopagwa kufanyika Julai 25 hadi 27 mwaka huu sasa limesogezwa mbele kutokana na sababu ambazo zipo nje ya uwezo wao,hivyo tamasha litafanyika Septemba 6 hadi 7 mwaka huu.
"Nitumie fursa hii kuwapa pole wananchi na wageni wetu ambao tuliwatarajia kushiriki kwenye tamasha letu kuja kujionea vivutio mbalimbali vya kitalii na majengo makubwa ambayo yalijegwa na mjerumani hususani jengo la Mkuu wa Wilaya ya Lushoto" amesema Kubecha.
0 Comments