About Me

header ads

DC AWATAKA TBA, DAWASCO NA TANESCO KUTATUA KERO ZA WAKAZI MAGOMENI KOTA

 

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Saad Mtambule (kushoto) akizungumza na wakazi wa Magomeni Kota katika mkutano wa kusikiliza kezo mbalimbali za wakazi hao jana jijini Dar es Salaam.



Bi. Mwajuma Hamis (mwenye kipaza sauti) mkazi wa Magomeni Kota akiwasilisha kero yake katika mkutano huo.

Mwenyekiti wa Kamati ya Wakazi wa Magomeni Kota, George Kasian akizungumza katika mkutano huo.

Baadhi ya wakazi wa Magomeni Kota wakiwasilisha kero zao katika mkutano na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Saad Mtambule (hayupo pichani).

Baadhi ya wakazi wa Magomeni Kota wakiwasilisha kero zao katika mkutano na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Saad Mtambule (hayupo pichani).

Mch. Peter Mkongo mkazi wa Magomeni Kota akizungumza katika mkutano huo.

MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Saad Mtambule ameutaka Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) kwa kushirikiana na Shirika la Usambazaji na Usimamizi Huduma ya Majisafi na Uondoshaji Majitaka (DAWASCO) pamoja na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuhakikisha wanatatua kero za wakazi wa Magomeni Kota jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Wilaya, ametoa agizo hilo jana alipokutana na wakazi wa Magomeni Kota katika mkutano wa kusikiliza kezo mbalimbali za wakazi hao ambazo zimekuwa zikilalamikiwa na wakazi hao, hasa za huduma ya maji safi na taka pamoja na huduma ya umeme.

Mhe. Mtambule, amewaagiza TBA na DAWASCO kuanza kazi maramoja ya kutatua changamoto ya huduma ya maji huku akiwataka Shirika la TANESCO kuanza kazi mara moja ya kuwasikiliza wananchi hao na kushughulikia kero zao za huduma ya umeme. 

"Nimekuja hapa leo kwa ajili ya kusikiliza changamoto mbalimbali ambazo wanazo wakazi wa hapa Magomeni Kota, ambao kuna Magorofa Matano yaliochukua Kaya 644...nimesikia kuna tatizo la maji ambayo yamekatwa kutokana na baadhi kugoma kulipia tozo za huduma (Service charge)...," alisema Mhe. Mtambule.

Akizungumza katika mkutano huo, Mwenyekiti wa Kamati ya Wakazi wa Magomeni Kota, George Kasian aliserma huduma za maji zimekatwa kwa wakazi hao kutokana na baadhi yao kugoma kulipia tozo za huduma jambo ambalo limekuwa likilimbikiza madeni na kuwa mzigo mkubwa, kabla ya jitihada za viongozi kushughulikia madeni hayo kulipwa.

Alisema wapo wakazi wa magorofa hayo ambao hadi leo hawajawahi kulipia gharama za 'Service charge' ambazo ndio zinazogharamia huduma za ulinzi, maji na usafi na kundi hilo la watu limekuwa likihamasisha wengine jambo ambalo limeleta mdororo wa uendeshaji majengo hayo hivyo kuomba msaada wa ofisi ya Mkuu wa Wilaya kuingilia kati.

Akiwasilisha kero, Bi. Mwajuma Hamis mkazi wa Magomeni Kota alisema mgogoro wa ulipaji huduma za maji katika eneo hilo umechangiwa na TBA kwani wamefunga mita mbili tu za utoaji huduma za maji kwa wakazi wote wa magorofa matano jambo ambalo bili inapokuja inakuwa kubwa na kutakiwa kuchangiwa na wakazi wote hivyo kuwa mgogoro.

"Mhe. DC chanzo cha mgogoro wa maji kukatwa kumesababishwa na TBA wenyewe hivi unafungaje mita mbili kwa kaya zaidi ya 644, ambapo kila mmoja anamatumizi yake, wengine mabaya wengine mazuri...bili ikitoka inakuja kubwa kila mmoja anabisha kulipa...hivi kwanini wasinge funga kila kaya ilipe bili yake, yaani mimi nilipe maji ambayo yametumiwa na mtu simjui ulisha wahi kuona wapi hiyo..?" TBA wamwtukosea sana kwanini wasitufungie kila mmoja na mita yake, mbona TANESCO wamefanya hivyo na hakuna mgogoro wa ulipaji umeme, hii sio sawa," alisema Bi. Hamis.

Aidha akijibu hoja hizo, Mkuu wa Wilaya aliwata TBA na DAWASCO kukaa chini na kuangalia namna ya kutatua changamoto hiyo, huku akisisitiza wakazi hao kulipa kwa wakati Service charge ili huduma zingine ziendelee hasa kipindi hiki ambacho taasisi hizo zinaangalia namna ya kutatua kero za wakazi wa eneo hilo.

"Serikali imetumia fedha nyingi kujenga nyumba hizi na mazingira yake sasa hatuwezi kuona baadhi yenu wanakwamisha kwa kugoma kutochangia 'Service Charge' ambazo ndio zimekuwa zikigharamia huduma za usafi, maji, ulinzi na mambo mengine...lazima kila mmoja wetu awajibike kulipa, hatuwezi kukubali baadhi yetu kukwamisha," alisema DC.

Post a Comment

0 Comments