About Me

header ads

KATIBU MKUU MAGANGA AIPONGEZA WCF KWA UTENDAJI UNAOFUATA VIWANGO VYA KIMATAIFA

 


Ataka WCF kukamilisha mchakato wa kupata Ithibati ya Viwango vya Kimataifa (ISO)

Na; Mwandishi Wetu – DODOMA



Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Bi. Mary Maganga ameupongeza Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) kwa utoaji huduma unaofuata viwango vya Kimataifa katika kushughulikia masuala ya fidia kwa wafanyakazi. 


Mhe. Maganga amebainisha kuwa, WCF tayari huduma wanazotoa zimekidhi vigezo vya Shirika la Kimataifa la Viwango ikiwa ni, menejimenti ya vihatarishi, Huduma mtandao,Tathmini ya kisayansi ya Takwimu bima na Kanzidata, hivyo ameutaka mfuko huo kuhakikisha unakamilisha mchakato wa kuipata ithibati ya viwango vya kimataifa (ISO) ili kuendelea kutoa huduma bora na kuboresha utendaji.


Ameyasema hayo Mei 6, 2024 alipotembelea Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), jijini Dodoma ikiwa ni sehemu ya ziara yaks ya kutembelea Taasisi zilizo chini ya Ofisi hiyo, ambapo amesema kuwa, Mfuko huo umekuwa ukitekeleza majukumu yake vizuri ikiwemo kulipa fidia kwa wafanyakazi walioumia, kuugua ama kufariki kutokana na kazi.


“Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) ni muhimu sana katika maeneo yetu ya kazi kwa sababu ni kiashiria kuwa serikali inatambua na kuthamini wafanyakazi nchini,” amesema


Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mfuko huo, Dkt. John Mduma amemhakikishia Katibu Mkuu kuwa Mfuko huo utakamilisha mchakato wa kupata Ithiubati ya  ISO na ameongeza kuwa tayari wamepata Tuzo ya Kimataifa   kwa utoaji Huduma mtandao na Shirika la Kazi Duniani (ILO) limeutambua muongozo wa Mfuko huo inaoutumia kufanya Tathmini ya viwango vya Fidia.


Katika hatua nyingine Dkt. Mduma amesema, Tathmnini ya uhai na uendelevu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), iliyofanywa na Shirika la Kazi Duniani (ILO) inaonesha kwamba Mfuko una uhimilivu (Sustainability) kwa kipindi cha miaka 30 kuanzia mwaka wa tathmini 2022/2023.



Menejimenti ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) na baadhi ya Watendaji kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu wakimsikiliza Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Bi. Mary Maganga (hayupo pichani) alipotembelea Mfuko huo tarehe 6 Mei, 2024.Mkurugenzi wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Dkt. John Mduma akieleza jambo wakati wa kikao hicho.

Baadhi ya Viongozi wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), wakiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya mfuko huo kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Bi. Mary Maganga alipotembelea Mfuko huo tarehe 6 Mei, 2024, jijini Dodoma.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Bi. Mary Maganga (katikati) akikabidhiwa maua kama ishara ya kumkaribisha katika Mfuko huo. Kulia ni Mkurugenzi wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Dkt. John Mduma. Kulia ni Bi. Navoneiwa Senkoro.

Picha ya pamoja ya Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Bi. Mary Maganga na viongozi pamoja na watumishi wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), wakati alipotembelea Mfuko huo tarehe 6 Mei, 2024, jijini Dodoma.
 

Post a Comment

0 Comments