Na Mwamvua Mwinyi,RufijiApril 23
Patrick Golwike (Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jamii wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Wenye Mahitaji Maalum [WMJJWM]) ameridhishwa na misaada inayoelekezwa na huduma zinazoelekezwa kwa akinamama waliojifungua na watoto waliokumbwa na maafa ya mafuriko Rufiji na Kibiti mkoani Pwani.
Aidha amepongeza mkoa,maofisa ustawi wa jamii kata,wilaya na mkoa kwa namna wanavyosimamia makundi ya Wanawake waliojifungua, wenye watoto na vijana wa kike ambao wapo kwenye ukuaji.
"Nichukue fursa hii pia kuwapongeza watalaam wa Maendeleo ya Jamii wakiongozwa na Afisa Maendeleo ya Jamii mkoa wa Pwani ambae ni mratibu wa Maafa Mkoa wa Pwani Roseline Kimaro ,ambao wamekuwa wakitekeleza jukumu la uratibu wa kuhakikisha waathirika wa mafuriko katika kambi Tano zilizopo kibiti na Ruiji wanapata huduma za msingi hasa wanawake ,watoto,wazee,na wenye mahitaji maalumu."alifafanua.
Hata hivyo kuhakikisha huduma za msingi zinatolewa kwa makundi hayo, mabinti balee kujilinda ,ulinzi wa watoto na kutoa elimu ya lishe na saikolojia .
Nae Mratibu wa maafa Roseline Kimaro alifarijika kuona wadau ambao wanapeleka misaada muhimu hasa kwa akinamama waliojifungua , watoto na mabinti balee.
"Ninawashukuru na umoja wa wanawake Tanzania, na mkoa kwa kujitoa kwao kupeleka mahitaji muhimu ya wanawake ikiwemo pedi,pempas,mabeseni,,nguo ,vyombo na vyakula kwani ni kama walijua kwamba ni moja ya changamoto ambazo ziliainishwa kuwakabili wanawake na watoto "alibainisha Roseline.
Roseline aliomba wadau wa jamii kuendelea kuwakimbilia kundi la wanawake, watoto,vijana na akinamama wajawazito na waliojifungua ili kuwapunguzia changamoto zinazowakabili.
0 Comments