VIONGOZI ya dini ya Kiislamu pamoja na waumini wa dini hiyo na wananchi kwa ujumla leo wameingia katika siku ya pili ya kuendelea na dua maalum ya kuliombea Taifa pamoja na viongozi wote.
Katka dua ya leo Ijumaa Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakari Bin Zubeir akiwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Jumanne Sagini pamoja na Mjumbe wa Halmashauri ya BAKWATA Ahmed Misanga ni miongoni walioshiriki katika dua hiyo.
Kwa mujibu wa ratiba imeelezwa kuwa leo Ijumaa ni siku ya pili ya mwendelezo wa wa dua hiyo kubwa iliyotangazwa kufanya na Mufti wa Tanzania kwa mfululizo wa siku tatu na kilele cha dua hiyo ni Februari 24 mwaka huu ambayo itakuwa Jumamosi.
0 Comments