Na Said Mwishehe, Michuzi TV
BENKI ya Maendeleo ya Kilimo(TADB) kupitia Mkurugenzi Mtendaji wake Frank Nyabundege imesema katika kipindi cha kuanzia Januari 2020 hadi Desemba mwaka 2023, benki hiyo imetoa mikopo yenye thamani ya Sh. bilioni 516.18 kwa njia ya moja kwa moja.
Akizungumza Mjini Tabora wakati wa ufunguzi wa ofisi ya benki hiyo Kanda ya Magharibi Mkurugenzi Mtendaji Frank Nyabundege amesema lengo la mikopo hiyo ni kuendeleza miradi ya kilimo, mifugo na uvuvi nchini.Mgeni rasmi katika ufunguzi huo alikuwa Waziri wa Kilimo Hussein Bashe.
Ambapo amesena katika fedha hizo za mikopo Sh. bilioni 448.25 imetolewa kwenye Kilimo mazao, Sh.bilioni 60.43 imetolewa kwenye mifugo,
na Sh.bilioni 7.50 imetolewa kwenye Uvuvi.
Ameongeza mikopo hiyo imetolewa kwenye miradi ya aina tofauti katika minyororo ya thamani 36 katika mikoa 27 na wilaya 125 nchini, ikiwemo vyama vya wakulima 151.
Kuhusu utekelezaji wa programu za kimkakati , Nyabundege amesema benki imeendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo inayohusisha ufadhili wa
Kilimo, Mifugo na Uvuvi; kutoa ushauri pamoja na kuwajengea uwezo wakulima na taasisi nyingine za fedha.
Amefafanua miradi hiyo ni Mradi wa Jenga Kesho Iliyo Bora “Building a Better Tommorow (BBT)", Programu ya Kopa Ng’ombe Lipa Maziwa Kupitia Mradi wa
Ti3P na Programu za Kujenga Uwezo (TA) wa Taasisi za fedha kukopesha kwenye Sekta ya Kilimo kupitia ufadhili wa AFD.
Pia Mradi wa Kusaidia Upatikanaji wa Zana Bora za Uvuvi (Boti na Vizimba), kwa Kutoa Mikopo Isiyo na Riba kwa kushirikiana na Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Programu ya Uanzishwaji wa Vutuo Jumuishi vya Kutoa Huduma za Zana za Kilimo (Mechanization Centers) kwa kushirikiana na AGITF.
Akizungumzia ukuaji wa benki hiyo Mwaka 2018, Serikali kupitia ofisi ya Waziri Mkuu iliipatia Benki mtaji wa Sh.Bilioni 57 ili kuiwezesha kutoa dhamana kwa wakulima, wafugaji, na wavuvi wadogo wadogo.
Amefafanua mpaka kufikia mwisho wa Desemba 2023, benki hiyo imefanikiwa kutoa udhamini kwa mikopo yenye thamani ya Sh bilioni 250.77 kupitia benki washiriki 16, na kiwango cha mikopo isiyolipika (NPL) ikiwa ni asilimia 0.
"Npenda kukufahamisha Waziri wa Fedha kuwa benki yetu inaendelea kutekeleza majukumu yake vyema na kwa mafanikio. Tangu Serikali ya Awamu ya Sita kuingia madarakani hadi kufika Desemba 31, 2023 Benki imeendelea kukua:
"Thamani ya mali za benki imeongezeka kutoka Sh.bilioni 362.8 mwaka 2021 na kufika Sh.bilioni 620.2 mwaka 2023 , hii ni sawa na ukuaji wa asilimia 70.9. Mizania ya mikopo imekuwa kutoka Sh.bilioni 120.8 hadi Sh.bilioni 330.8 mwaka 2023, hii ni sawa na ukuaji wa asilimia 173.84, " amesema.
Pamoja na hayo amesema ofisi za kanda zimeongezeka kutoka tatu mwaka 2021 hadi ofisi saba mwaka 2023.Kanda hizo ni Kanda ya Ziwa inayojumuisha Mwanza, Kagera, Shinyanga, Simiyu, Mara, na Geita.
Kanda ya Kati Dodoma inajumuisha Dodoma na Singida wakati Nyanda za Juu Kusini ni mikoa ya Mbeya, Iringa, Songwe, Njombe, na Rukwa. Kanda ya Mashariki inahusisha mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Morogoro, na Zanzibar Kanda ya Kusini ni Mtwara, Lindi na Ruvuma.
Amesema Kanda ya Kaskazini inahusisha mikoa ya Arusha Manyara, Kilimanjaro, na Tanga wakati Kanda ya Magharibi Tabora Katavi na Kigoma."Hii inaonesha nia ya Benki ya kusogeza huduma zake karibu zaidi na wananchi, hasa wakulima, wafugaji, na wavivi kote nchini."

Waziri wa Kilimo Husen Bashe akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Kilimo nchini(TADB)Frank Nyabundege mara baada ya kuwasili wakati wauzinduzi wa Tawi la benki hiyo mkoani Tabora.
0 Comments