Na Dotto Mwaibale, Singida
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida, Martha Mlata (pichani) kesho Julai 3,
2023, anatarajia kuwasha moto wakati atakapo kuwa katika ziara yake ya kikazi
katika Wilaya ya Singida ya kukagua miradi ya maendeleo na kuzungumza na
wananchi.
Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ziara
hiyo, Katibu wa CCM Wilaya ya Singida Shabani Hamisi alisema ziara hiyo katika
wilaya hiyo ni ya muhimu sana kwao.
"Ziara hii aatakayoianza kesho mwenyekiti
wetu wa chama mkoani hapa ni ya muhimu sana kwa ajili ya kukihimarisha
chama," alisema Hamisi.
Akizungumzia mambo atakayoyafanya wakati wa ziara
hiyo alisema atatembelea Balozi Shina namba tisa lililopo Kitongoji cha
Mnung'una ambapo pia atapata fursa ya kuzungumza na wananchi wakiwemo Wana CCM
na kupata taarifa ya chama.
Alisema kazi nyingine ambayo ataifanya ni
kutembelea miradi ya maendeleo inayotekelezwa wilayani humo na moja ya miradi
hiyo ni ujenzi wa shule za Boost uliopo
Kata ya Minga na ujenzi wa Barabara ya kiwango cha lami na kufanya
mkutano wa hadhara na wananchi wa kata hiyo.
Hamisi alisema katika ziara hiyo Mlata ataongozwa
na wajumbe wa kamati ya siasa ya wilaya hiyo chini ya Mwenyekiti Lusia Mwiru.
Mwenyekiti huyo wa chama mkoani hapa Martha Mlata ataendelea na ziara hiyo katika wilaya ya Mkalama atakayoifanya Julai 4, 2023, Iramba, Julai 5, Ikungi Julai, 6, Singida Vijijini, Julai 7 na kumalizia katika Wilaya ya Manyoni Julia 8 na 9.
0 Comments