Katibu Mtendaji wa Tume ya kurekebisha Sheria Tanzania (LRCT) , Bw. Griffin Mwakapeje akizungumza wakati wa Kikao cha Menejimenti ya Taasisi hiyo kilichofanyika leo Julai 6, 2023 katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za tume hiyo jijini Dodoma.
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
KATIBU Mtendaji wa Tume ya kurekebisha Sheria Tanzania (LRCT) , Bw. Griffin
Mwakapeje amesema Tume ipo kwenye mchakato wa kutekeleza Mpango wa kushirikisha vyuo vikuu mbalimbali
hapa nchini katika mashindano ya Uandishi wa Insha za masuala mbalimbali ya Kisheria
na yenye changamoto katika jamii ili
waweze kushiriki na kuchangia katika utaratibu wa marekebisho ya sheria kwenye
maeneo husika.
Maelezo hayo ameyatoa wakati wa Kikao Cha menejimenti ya Taasisi hiyo
kilichofanyika leo Katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi za Tume hiyo ambapo
ameeleza kwamba yapo matukio mbalimbali yanayoibuka Katika jamii yenye
mueonekano wa kisheria ambapo zikiandikwa Insha zinaweza kuisaidia Tume kupata
taarifa za kitafiti.
Amesema kazi hiyo ya Uandishi wa Insha kwa wanafunzi itasaidia kuwajengea wanafunzi hari ya
kufanya utafiti na kuiwezesha Tume kupata
taarifa mbalimbali zitakazofanyiwa kazi Kwa kina na wataalamuwa Taasisi
hiyo, Jambo ambalo litaongeza ufanisi wa Tume na maboresho ya sheria.
Aidha ameeleza kwamba washindi wa Insha watapatiwa zawadi mbalimbali
zikiwemo fedha taslimu, kuchapishwa kwa maandiko yao kwenye
jarida la tume, pamoja na vyeti na kwamba zoezi hilo litaongeza hamasa kwa wanafunzi kuwa wazalendo Katika
nchi yao.
"Tutafanya makubaliano na vyuo mbambali hapa nchini kuhusu Uandishi wa
Insha ili kuwa na uratibu mzuri wa zoezi hili ikiwa ni pamoja na kuwahamasisha
wanafunzi kufanya utafiti wa masuala mbalimbali ya kisheria yanayogusa jamii
ili mwisho wa siku maandiko hayo
yasaidie kufanya maboresho ya Sheria
husika.
Katika kikao hicho, Bw. Mwakapeje amewahimiza wataalam na watumishi kuongeza jitahada kwenye utekelezaji wa majukumu na kuwataka wawe wabunifu ili kuyafikia malengo yao.
0 Comments