About Me

header ads

WADAU WA MADINI YA TANZANITE WATAKA HOSPITALI, MAJI NA BARABARA MACHIMBONI

 

Na Mwandishi wetu, Mirerani

WADAU wa madini ya Tanzanite wa mji mdogo wa Mirerani wilayani Simanjiro mkoani Manyara, wameiomba serikali kuwezesha ujenzi wa hospitali, kituo cha afya au zahanati kwani machimbo hayo hayana huduma za afya, kuwavutia maji na pia miundombinu ya barabara.

Kutokana na serikali kupata mamilioni ya fedha kupitia kodi inayopatikana kwenye madini ya Tanzanite inapaswa kuwekeza huduma za afya, maji na miundombinu ya barabara kwa manufaa ya wadau wote wa madini hayo.

Mdau wa madini ya Tanzanite, Hawa Kiranga, akizungumza mji mdogo wa Mirerani kwenye warsha ya mradi wa Tanzanite kwa uchumi imara wa mwanamke ulioandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la Civil social protection foundation (CSP) amesema serikali inapaswa kufikisha huduma hizo kwa jamii.

Hawa amesema serikali inapata fedha nyingi kupitia kodi ya madini ya Tanzanite hivyo ingerudisha kwa jamii kwa kujenga, zahanati, kituo cha afya au hospitali.

Mdau mwingine wa madini hayo Fatuma Kifunta amesema serikali ikamikishe soko la madini Mirerani ili jamii hasa wanawake waweze kufaidika na mnyororo wa thamani wa madini ya Tanzanite.

"Wanawake wajasiriamali wanaopanda kwenye migodi ya madini ya Tanzanite wanakwenda umbali mrefu wengi wao wanatembelea umbali mrefu ila soko lingekuwa hapa Mirerani wasingepata changamoto hiyo," amesema Fatuma.

Mdau mwingine Tausi Bakari amesema serikali inapaswa kuweka miundombinu rafiki kwenye machimbo hayo ikiwemo barabara zilizopo ndani ya ukuta unayozunguka migodi ya Tanzanite.

"Barabara ni mbovu, watu wanatumia pikipiki hakuna magari ya abiria, pia maji hakuna, serikali ivute maji kwenye machimbo kwani haya ya kupelekwa na magari yanauzwa kwa bei ghali," amesema.

Mwanasheria wa CSP, Eliakim Paulo amesema kongamano hilo la mradi wa Tanzanite kwa uchumi imara wa mwanamke linahusisha wanawake wadau wa madini hayo, wasaidizi wa kisheria na waandishi wa habari.

Paulo amesema mradi wa Tanzanite kwa uchumi imara wa mwanamke, unahusisha wanawake wajasiriamali wa madini hayo wa kata za Mirerani, Endiamtu na Naisinyai wanaofanya biashara zao ndani ya ukuta unayozunguka migodi ya Tanzanite.

"Lengo ni kusababisha uchechemuzi kwenye kongamano hili na pia waandishi wa habari wataingia ndani ya ukuta unayozunguka migodi ya Tanzanite ili kuona changamoto na mafanikio ya wanawake hao," amesema.

Kaimu ofisa mtendaji mkuu wa mamlaka ya mji mdogo wa Mirerani (TEO) Isack Mgaya akifungua kongamano hlo la siku nne ameipongeza CSP ambayo imeandaa mradi huo wa Tanzanite kwa uchumi imara wa mwanamke.








Post a Comment

0 Comments